November 07, 2013

ELIMU YETU MIKONONI MWA SHETANI


MARKUS MPANGALA (DAR ES SALAAM) NA HAPPY JOSEPH (CHANGCHUN, JILIN (CHINA).

WAKATI mwingine tunatakiwa kulalamika ka kila jambo kutokana na muktadha halisi. Tunapaswa kupiga kelele hata kama hazitakuwa na ufumbuzi, lakini angalau itakuwa inaweka rekodi sawa kwamba uamuzi uliochukuliwa hakuwa sawa. Kila mmoja anaweza kulalamika, na serikali inaweza kutuona  walalamishi zaidi, lakini kwangu mimi hili ni zaidi ya ulalamishi. Ni zaidi majuto. Ni zaidi hisia kali, kwamba tunajenga elimu ya namna gani kwa kizazi kijao. 
HAPPY JOSEPH katika pozi. Huyu ndiye nimeshirikiana naye kuandika makala hii kuhusu Elimu. Asante rafiki yangu kwa mawazo mazuri.
Kwanza tulianza kulalamikia eti kwamba mitihani ya kidato cha nne kuna watu wanapendelewa. Baadhi ya watanzania wenzetu wakapayuka mpaka kutoa povu midomoni ati mfumo wa elimu unawapendelea jamii au watu wa imani fulani. Kwangu mimi huu ulikuwa ujumbe tosha, matatizo yaliyolimbikizwa sasa yamekuwa shubiri na kusababisha kushindwa kufikiri sawasawa. 

Matatizo tuliyyalea kwa miaka mingi yamesababisha kutafuta majibu mengine ambayo hayana kichwa wala miguu. Matatizo ambayo yamelelewa kwa ustadi na kukabidhiwa mikononi mwa shetani (ujinga). Waama, elimu yetu tumeipeleka mikononi mwa shetani na hilo hakika sitachelea kusema. Akindika kwenye kitabu chake cha ‘Mwalimu Mkuu wa Watu,” Mzee wetu Pacsally Mayega, anasema, “Ndani ya kichwa mvivu ni karakana ya shetani, na mtu mvivu ni kama jiwe lililopakwa mav,”. 

Ni maneno mazito ambayo yanavuta hisia zangu kuona serikali yetu tukufu inadhani ‘Divison V’ ni moja ya ujanja mbovu kuboresha elimu yetu, badala ya kusema ukweli kwamba hilo ni daraja sifuri kwa watui waliofeli. Tabu ya nini kufika hili? 

Kwanini swerikali inajibebesha mzigo mzito kama huu? Naam, tuko mikononi mwa shetani, huku Bunge letu tukufu likiidhinisha watanzania kufikishwa kwenye pango la shetani. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa Sifuni Mchome alitutangazia madaraja mapya kwa mtazano wa serikali. 

Zamani tulikuwa na  A=80-100, B=65-79, C=50-64, D=35-49, F= 0-34 kwa upande wa kidato cha sita A=80-100, B=75-79, C=65-74, D=55-64, E=45-54, S=40-44 na F= 0-39. Naam, sasa serikali yetu sikivu imesema madaraja yatakuwa hivi; A=75-100, B+=60-74, B=50-59, C=40-49, D=30-39, E=20-29 na F=0-19, huku serikali hiyo ikisema kuwa daraja sifuri limeondolewa ili kuweka mlolongo mzuri. 

Waaooooo! Tumefika mahali kudhani mlolongo mzuri ndiyo mazingira mazuri. Tunashindwa kutibu maradhi na kuongeza ugonjwa mzito, ambao utatuchukua muda kuondokana nao. Kwamba shida yetu ilikuwa mlolongo mzuri ama tunatakiwa kupewa elimu bora?
Ni  kweli kwamba serikali imefanya vizuri kutuanzishia sekondari sisi watoto wa masikini tuliokulia ukanda wa ziwa Nyasa na wengineo kote nchi. Shule za Kata ingawa baadhi yetu hatukusoma lakini imewasaidia wale tuliowaacha nyuma kwani angalau wamepata elimu hata kama haina ubora unaotakiwa. 

Serikali ya CCM imeamua kwa dhati kabisa kutupeleka katika dimbwi la tabasamu la shetani na kudhani inaokoa kizazi hiki. Nchi yetu imeuwa ikijikita sana kwenye suala la Ilani za chama kama msingi wa maendeleo badala ya sera. 

Kilichosababisha kufutwa mitihani ya kidaoto cha nne ilikuwa Ilani ya CCM si sera ya Taifa letu. Kufutwa matokeo hakukuwa na maana kutabadilisha lolote kwani serikali yenyewe imejenga mazingira ya kila ya namna ya kuwa mchochezi namba moja kwa wananchi.
Katika hoja hii nilikumbuka maneno mazito ya rafiki yangu Happy Joseph aliyeko masomoni mjini Changchun, Jilin, nchini China akisema, “Hivi kama kocha ameona timu yake haifanyi vizuri (wachezaji wanapiga mashuti nje ya magoli), ataamua kupanua maagoli katika uwanja wa mazoezi? Je, katika mashindano na timu nyingine katika uwanja mwingine ategemee nini? 

Anaongeza kwa kusema, “Elimu ya sasa katika utandawazi huu si ya nchi Fulani, inapaswa kuwa na viwango vya kimataifa. Lazima mtu ashindane na wa mataifa mengine. Tanzania haiwezi kuwa na elimu yap eke yake, ndio maana tunapigwa change macho kwenye mikataba na mataifa mengine,”

Kama walivyo wadau wengine rafiki huyo huyu anatoa ushauri kwa serikali akisema, “Kwanza, Serikali ikae na wadau wa elimu kupitia tafiti za kielimu zilizofanywa na taasisi mbali mbali mfano Haki Elimu kuona matatizo ya elimu ni yapi, na mbinu gani zitumike kupandisha kiwango cha elimu  na si idadi ya ufaulu hewa. Pili, Serikali kuwekeza zaidi katika elimu; hakuna aisyefahamu kuwa hakuna Maabara, Maktaba, na walimu wenye nia katika shule za umma. Tatu,  Serikali itazame upya mtaala wa elimu, isiung'ang'anie, pia itazame mfumo wa elimu, kwamba ipi iwe lazima na ipi iwe ziada.

Aidha, anasema, serikali itazame maslahi ya Walimu na ubora wake.  Katika pendekezo hilo la mwisho ndiyo linanipa simanzi. Kwamba kujali maslahi ya Walimu ni suala gumu ambalo serikali imeshindwa kisheria na kiakili pia. Inaudhi kusema maneno hayo lakini hakuna namna nyingine, kwamba serikali imeshindwa kisheria japo iliagizwa hivyo na Mahakama Divisheni ya Kazi wakati ilipozuia mgomo wa Walimu kote nchini. Katika majadiliano yake na Chama cha Walimu, ilikubaliwa kuwa serikali itaongeza mishahara kwa kiwango cha asilimia 67. 

Lakini katika hali ya kustaajabisha serikali haikufikia kiwango hicho, bali ilikomea kwenye asilimia 24. Katika mkutano na waandishi wa Habari miezi kadhaa iliyopita, Rais wa Chama cha Walimu nchini, Gratian Mkoba alisema kuwa jambo hilo liliwasikitisha walimu huku serikali ikianza harakati za ‘Big Results Now’ ambayo iliitongoa huko Malaysia. 

Nia nzuri ya serikali haibezwi, lakini kinachogomba ni mtindo unaotumika kuendelea kuwategemea walewale wanaonyonywa na kudhani wanaweza kuleta mapinduzi. Walimu ndio wahanga wa unonyaji unaofanywa kwani kwa mujibu wa mazungumzo ya mezani kati yao na serikali ilikubaliwa malipo yao yafikie asilimia 67 kwa kile kilichoeelezwa kuwa nchi yetu haina fedha za kutosha. 

Labda, lakini kuomba kufika asilimia 67 kisha kushindwa kutimiza bila sababu zozote hakuna jingine zaidi ya kufikisha elimu mikononi mwa shetani. Mikono ambayo bila shaka itatuzalishia magaidi kutokana na ukosefu wa elimu wmafaka na yenye tija kwa maslahi ya taifa letu. Ni hatari kuichezea elimu kwa kiwango hiki halafu tukatarajia kukutana na wanazuoni waliokomaa. Asenteni kwa kunisoma.
Baruapepe; mwanazuoni27@gmail.com

@MAKALA HII IMECHAPISHWA GAZETI LA RAI, Novemba 7, 2013.

November 05, 2013

DC MUHINGO: TAMASHA LA HANDENI NI FURSA YA KIMAENDELEO



Na  Mwandishi Wetu, Handeni
MKUU wa wilaya Handeni, DC Muhingo Rweyemamu, amewataka wananchi wa Handeni, mkoani Tanga kulitumia Tamasha la Handeni linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 mjini hapa kwa ajili ya kutafuta fursa za kimaendeleo na kuwapatia maisha bora Watanzania wote kwa kupitia sekta ya utamaduni.

Akizungumza jana mjini Handeni, Muhingo alisema kutokana na tamasha hilo kufanyika mwisho wa mwaka, Desemba 14, itakuwa chachu ya kuwaunganisha watu wote, sanjari na kujadili changamoto zinazoikabiri Handeni na Tanzania kwa ujumla.

Muhingo alisema kuwa tamasha hilo lina umuhimu mkubwa kutokana na kuandaliwa maalum kwa ajili ya Watanzania kwa ajili ya kuangalia ngoma na matukio mbalimbali ya kijamii.

“Wakati napongeza kwa dhati kuandaliwa kwa tamasha hili wilayani hapa, pia nawaomba watu waje kwa wingi kushuhudia namna gani Handeni imepiga hatua kimaendeleo na kuangalia namna gani wanaweza kusonga mbele.

“Naamini tutafikia hatua nzuri kwa kushirikiana na wadau wote, hivyo wale wanaoishi mbali na Handeni pia ni wakati wao kurudi nyumbani mwishoni mwa mwaka kujifunza mambo ya utamaduni wao, sanjari na kufanya juhudi za kupiga hatua kimaendeleo,” alisema.

Tamasha hilo linaloandaliwa na Mratibu wake Kambi Mbwana, hadi sasa limedhamiwa na Phed Trans, Clouds Media Group, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group.

Wengine ni duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com, huku likipangwa kuanza saa 2 za asubuhi hadi saa 12 za jioni.

November 04, 2013

HONGERA MDAU WETU WA WILAYA YA NYASA

VITUS MATEMBO ametunukiwa shahada yake ya kwanza ya chuo kikuu aliyohitimu karibuni na sherehe kufanyika huko Moshi, mkoani Kilimanjaro. Tunamtakia mafanakio mema na ataendelea kutuhabarisha mambo mengui kuhusu Wilaya ya Nyasa

TAMASHA LA UTAMADUNI HANDENI NA MIPANGO KABAMBE YA KIMAENDELEO




Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ILI kujenga jamii bora na yenye kujua tamaduni zao, kunahitajika kuandaliwa matamasha muhimu yenye dhamira ya kweli katika kona mbalimbali za nchi yetu. Huo ni mpango mzuri na wenye tija.


Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani.

Katika suala hilo, wale wadau wanaotarajia au waliowahi kuandaa matamasha ya aina hiyo ni dhahiri wanatakiwa waungwe mkono badala ya kukatishwa tamaa.
Kwa sasa, tamasha ambalo linatajwa katika vinywa vya watu wengi ni lile la Handeni, linalotarajiwa kufanyika Desemba 14, wilayani Handeni mkoani Tanga.

Tamasha hilo la utamaduni na michezo linatambulika kwa jina la ‘Handeni Kwetu,’ jina lililotokana na mtandao ‘blog’ ya Handeni Kwetu.
Mratibu wa Tamasha la Handeni, Kambi Mbwana, pichani.
Vyovyote litakavyotajwa na wadau wa matamasha duniani kote, ili mradi linatimiza na kutoa majibu halisi ya namna ya kutangaza na kukuza utamaduni wa Tanzania, si vibaya na njia ya kulitangaza mbele ya jamii.

Katika mazungumzo yaliyofanyika mapema wiki hii, mwishoni mwa wiki iliyopita, Mratibu Mkuu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana, anasema kuwa lengo la kuandaa tamasha hilo ni kushirikiana na serikali na wananchi wote kujua mbinu imara za kuutangaza utamaduni wetu.


Mbunge wa Handeni na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Abdallah Kigoda, pichani.
Anasema kwa maeneo kama Handeni na kwingineko, kumekuwa na changamoto kubwa za wananchi kuacha utamaduni wao na kufuata wa wenzao jambo linalotakiwa lipingwe vikali.

“Nilikaa chini na kutafakari namna gani ya kuwaunganisha watu wote katika tukio moja na kuwa sehemu ya wao kuangalia ngoma zetu, nyimbo zetu na mbinu za kijamii kwa ujumla wake.

“Naamini katika umri wa taifa letu la Tanzania, kuna mengi yametokea na yaliwahi kutokea hasa wakati wa ukoloni, hivyo naamini siku hiyo tutajua ni kiasi gani watu wa asili ya Handeni walikuwa na mchango kwenye jamii yao,” alisema Mbwana.

Mbwana ambaye ni mwandishi wa habari na mmiliki wa ‘blog’ ya Handeni Kwetu (www.handenikwetu.blogspot), anasema kwamba kwa kukutana watu wote ni sehemu ya kuangalia namna ya kulitumikia taifa letu la Tanzania na kubuni mbinu za kujikomboa kiuchumi.

Mdau huyo wa mambo ya utamaduni, michezo na sanaa kwa ujumla wake ukiwamo muziki, anasema kwamba Handeni ni miongoni mwa wilaya zenye changamoto kubwa hivyo kuna haja ya wadau wote kukutana kwa pamoja na kuangalia namna ya kuzitatua, hasa kwa kupitia tamasha hilo.

“Huu si wakati wa kuangalia Mkuu wa Wilaya (DC) Muhingo Rweyemamu anafanya nini au Mbunge Abdallah Kigoda na viongozi wote wa serikali, ila jambo la muhimu ni kushirikiana nao kuleta maendeleo.
“Mtu wa kwanza katika maendeleo ni mwananchi mwenyewe, hivyo naomba kuwakaribisha Watanzania na hata wale wasiokuwa Watanzania kukutana pamoja na sisi kwenye tamasha hili,” alisisitiza Mbwana.

Aidha, Mbwana anatumia muda huo kuwaomba wadau wote, wakiwamo viongozi wa serikali, mashirika na kampuni kujitokeza kudhamini tamasha hilo litakalokuwa la aina yake. Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu linafanyika kwa mara ya kwanza, likipangwa kuanza saa tatu asubuhi hadi saa 12 jioni, ambapo vikundi mbalimbali vya sanaa vitashiriki.

Ili kuleta hali ya kimkoa, Mbwana anasema juhudi zinafanyika kupata vikundi katika baadhi ya wilaya za Mkoa wa Tanga ili kuimba nao, kucheza nao na kushiriki nao katika jambo la kimaendeleo. Mdau huyo wa habari anasema kwamba hadi sasa wadau kadhaa wamejitokeza kudhamini tamasha hilo linalotikisa katika maeneo ya Handeni na Tanzania kwa ujumla.

Anawataja wadau hao kuwa ni pamoja na Yusuphed Mhandeni, ambaye ni Mchumi wa CCM Kata ya Makumbusho kwa kupitia Kampuni yake ya Yusuphed Trans, yenye magari yanayotoka Dar es Salaam kwenda Mkata, wilayani Handeni, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group.

Wengine ni duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com.

Mbwana anasema kwamba kwa kupitia tamasha hili, wadau wote watapata fursa ya kutangaza biashara zao, ukizingatia kuwa tamasha hili linatarajia kukutanisha watu wengi zaidi sehemu moja. “Tunaomba udhamini kwa watu wote ili tushirikiane katika kufanikisha tamasha hili la kihistoria, huku tukiamini kuwa wenzetu wa Kilindi, Korogwe tutakuwa nao pamoja.

“Maandalizi yanaendelea kuhakikisha kuwa tunafanya kitu cha tofauti katika tamasha hilo, nikiamini kuwa mguso huu utaendelea kushika kasi na habari hizi njema kuenea nchini kote,” alisema. Mbwana anasema kwamba wazo la kufanyika kwa tamasha hilo limepewa baraka na viongozi wote, akiwamo DC Rweyemamu na Mbunge, Abdalah Kigoda, ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara.

Anasema kuwa kwa kufanyika kwa tamasha hili ni muendelezo wa mipango mingi mizuri ya kimaendeleo itakayoandaliwa kwa kushirikiana na Watanzania wote, hususan wananchi wa Handeni. Mwisho kabisa Mbwana alitumia muda huo kuwakumbusha wafanyabiashara mbalimbali wilayani Handeni na Tanga kwa ujumla, kuingia moja kwa moja katika tamasha hili la aina yake.

HOJA YANGU TETE KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYASA



NA MWANDISHI WETU, MBAMBA BAY

Nakushukuru kwa kuanzisha Geti la ukaguzi wa bidhaa  zinazotoka Nyasa kwenda sehemu nyingne. Geti lipo NANGOMBO, Najua walinzi hawalali, wakuu wa idara zote wamewekeana zamu kulala getini. NI MWANZO MZURI KWA WILAYA yetu.kwani mapato yatakuwa mengi, hvyo kuleta Maendeleo kwetu Nyasa. ILA WENGI YA WAFANYAKAZI PALE GETINI NI WALAJI WA HELA, 

Pia kinachopatikana pale naskia ni tofauti na kwenye vitabu vya halmashauri. MWISHO naomba waondoe unyanyasaji kwani mtu akibeba samaki/dagaa wa mboga ni lazma alipie, maembe matano ni shda, au hata dumla 4 za mihogo analipia kweli ni haki?. Wakati wafanyakazi wengi wanabebelea vyakula vingi toka nyasa na magari ya serikali aina ya STK,SM,STJ, DFP na hawalipishwi KWA NINI?.