November 04, 2013

HOJA YANGU TETE KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYASANA MWANDISHI WETU, MBAMBA BAY

Nakushukuru kwa kuanzisha Geti la ukaguzi wa bidhaa  zinazotoka Nyasa kwenda sehemu nyingne. Geti lipo NANGOMBO, Najua walinzi hawalali, wakuu wa idara zote wamewekeana zamu kulala getini. NI MWANZO MZURI KWA WILAYA yetu.kwani mapato yatakuwa mengi, hvyo kuleta Maendeleo kwetu Nyasa. ILA WENGI YA WAFANYAKAZI PALE GETINI NI WALAJI WA HELA, 

Pia kinachopatikana pale naskia ni tofauti na kwenye vitabu vya halmashauri. MWISHO naomba waondoe unyanyasaji kwani mtu akibeba samaki/dagaa wa mboga ni lazma alipie, maembe matano ni shda, au hata dumla 4 za mihogo analipia kweli ni haki?. Wakati wafanyakazi wengi wanabebelea vyakula vingi toka nyasa na magari ya serikali aina ya STK,SM,STJ, DFP na hawalipishwi KWA NINI?.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako