June 27, 2014

SAKATA ESCROW-TUHUMA ZA UFISADI



Na Mwandishi Wetu, FACULTAS

Sakata la Ufisadi wa Bilioni 200 kupitia Akaunti ya Escrow limeibuka tena bungeni baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila kuomba muongozo na kutaka kiti cha Spika kutoa umuzi wa suala hilo ili kufikia muafaka huku akimtuhumu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema kumtamkia maneno ambayo yanatishia uhai wa maisha yake.

Sakata hilo limekuwa likizua malumbano makali bungeni kufuatia baadhi ya wabunge kulitaka bunge kuingilia kati na kutolea msimamo suala hilo badala ya kuiachia Takukuru na CAG kuchunguza pekee.
Kafulila anasema Bunge linawajibu wa kusimamia serikali na kwamba kuna haja ya kutoa Msimamo wake kuhusiana na sakata zima la Akaunti ya Escrow iliyofunguliwa kufuatia mgogoro baina ya Tanesco na Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL baada ya pande hizo mbili kushindwa kukubaliana kwenye malipo ya umeme kupitia mkataba uliosainiwa na pande zote Mei 26,1995.

Katika kipindi cha maswali na Majibu Mbunge wa Viti Maalumu Leticia Nyerere anaulizia mpango wa Serikali wa kulipa fidia watanzania wanaopata madhara yatokanayo na matumizi ya simu zisizo na viwango vya ubora.

Ni mkutano wa 15 kikao cha 42 cha Bunge la bajeti ambapo mbali na kipindi cha maswali na majibu bunge pia limejadili Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2014.

NINI MAONI YAKO?
©FACULTAS, 2014

No comments:

Post a Comment

Maoni yako