September 29, 2017

KWA WAANDISHI WA VITABU NA MACHAPISHO MENGINE YA KISWAHILI.

NA MAUNDU MWINGIZI

Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), kwa mujibu wa sheria ndio chombo, kwa niaba ya serikali, kinachosimamia masuala yote yanayohusu lugha ya Kiswahili Tanzania. Kwa miezi kadhaa sasa limekuwa likiandaa kanuni mpya za Kiswahili Tanzania. Rasimu ya kanuni hizo imeshakamilika na baadhi ya wadau walipewa kuisoma na kutoa maoni yako, na baadaye wadau wachache walialikwa kwenye kikao kingine cha kupitia maoni yaliyotumwa na wadau juu ya rasimu hiyo. 

Wajumbe wa kikao wengi waliwakilisha wenzao kutoka sekta ndogondogo zinazogusa lugha ya Kiswahili. Mfano, Watunzi wa vitabu, waandishi wa habari za Kiswahili, Bodi ya filamu Tanzania, Wakalimani/Wafasiri wa kawaida na wale wakalimani wa lugha za alama, walimu wa Kiswahili kwa wageni, watu wa matangazo, wawakilishi kutoka vyuo vikuu, watu wa mashairi n,k. 



Kwa bahati nilikuwa mmoja wa wajumbe wa kikao hicho cha mwisho, nikiwakilisha wanaofundisha Kiswahili kwa wageni. Inasemekana baada ya kikao kile rasimu ile itakwenda kwa waziri husika kwa ajili ya utiaji saini ili utekelezaji uanze maramoja.

Kwa muhtasari ni kwamba:
1. Mtu yeyote anayejishughulisha na lugha ya Kiswahili mfano awe mtunzi/mwandishi wa vitabu, mhariri wa vitabu, mkalimani/mfasiri, mkalimani wa alama, mwalimu wa Kiswahili kwa wageni, lazima:
a) Apate kibali kutoka BAKITA ambacho atakuwa akikilipia kwa mwaka
b) Awe na shahada ya Kiswahili
c) Awe na nambari ya mlipa kodi na cheti cha kuonesha kwamba hadaiwi kodi
d) Awe tayari kufanyiwa ukaguzi wakati wowote inapohitajika
2. Mtu yeyote anayendika kitabu/chapisho lolote la Kiswahili, tangazo (Bango), au la redioni, tv, lazima apate tangazo au andiko lake lihakikiwe na lilipiwe na BAKITA kabla kutolewa
3. Maelezo yaliyomo katika dawa au vipodozi vya ndani na nje, lazima yawe katika lugha ya Kiswahili, yahakikiwe na yalipiwe kabla kuwekwa sokoni kwa walaji.

NB: Jana vyombo vya habari vimeripoti kitu kama hiki (Kanuni Mpya) kwenye tasnia ya habari pamoja mitandao ya kijamii.

Nimeituma kama nilivyoipokea. 

Nini maoni yako?!

No comments:

Post a Comment

Maoni yako