Mara baada ya Jaji wa Mahakama
ya Juu kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi, Raila Odinga alizungumza na vyombo
vya habari na kueleza mambo yafuatayo.
1.Aliishukuru Mahakama ya Juu
kwa kuzingatia sheria na kubatilisha matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika
Agosti 8 mwaka huu.
2. Alitoa shukrani kwa Majaji
wawili walipinga kurudiwa uchaguzi huo, Jaji Njoki Ndungu na Jaji JB Ojwang
kwasababu walisimamia wanachokiamini.
3. Amethibitisha kuwa Tume ya
uchaguzi IEBC imekuwa ikikiuka kanuni na taratibu za uchaguzi wakati wa
kuhesabu kura za urais.
4. Baada ya ushindi, Raila
alikwenda kuipongeza timu ya Mawakili wake James Orengo (Seneta wa Siaya ) na
Otiende Omollo.
5. Nafasi ya waangalizi wa
kimataifa wa uchaguzi inatakiwa kuwekewa mtazamo mpya kwasababu wanaweza
kuhongwa.
6. Waangalizi wa kimataifa
waliokuwa bega kwa bega na NASA wameuangusha upinzani nchini humo na walikuwa
na lengo la kutafuta umaarufu tu.
7. Kuna umuhimu na kila sababu
ya kuangalia nani atakuwa msimamizi wa uchaguzi wa marudio utakaofanyika ndani
ya siku 60 baada ya hukumu ya mahakama.
8. Amependekeza Makamishna na
maofisa wa Tume ya uchaguzi IEBC na Mkurugenzi mtendaji wanapaswa kushtakiwa.
9. Ni muhimu kufanya ukaguzi
katika mifumo ya mawasiliano ya Tume ya IEBC.
10. NASA inatarajia kuona
mabadiliko katika uchaguzi ujao.
©Nishani Media,
Dar es salaam
4/9/2017
No comments:
Post a Comment
Maoni yako