NA MWANDISHI WETU
MTU mmoja aliyetambulika kwa jina la Gaudansi Kapinga(31)
aliyekuwa Mkazi wa Kijiji cha Mbuyule Tarafa ya Ruhekei wilayani Nyasa mkoani
Ruvuma,ameuawa kwa kupigwa na mawe hadi kufa na wananchi wa kijiji hicho.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma SACP Gemini Mushi
(pichani) amesema tukio lilitokea Novemba 2,2017,majira ya saa mbili usiku katika kijiji
hicho ambapo watu wasiofahamika walijichukulia sheria mkononi na kumua marehemu
huyo.
Kamanda Mushy amebainisha kuwa inadaiwa katika tukio
hilo,marehemu anadaiwa kukutwa akivunja duka la Furaha Matembo na kwamba
upelelezi wa kina unaendelea kufanywa na Jeshi la polisi pamoja na kuwasaka
watuhumiwa wa tukio hilo.
Katika tukio jingine lililotokea jana majira ya saa nne
usiku,Kamanda Mushi amesema Jeshi la
Polisi limewakamata watu saba katika Mtaa wa Misufini wilayani Tunduru wakiwa
na kiasi cha lita sita za pombe haramu aina ya gongo.
Kamanda Mushi anatoa raia kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma
kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi,badala yake wawafikishe watuhumiwa
katika vyombo vya sheria na kwamba waache biashara haramu ya gongo kwa sababu
serikali itawachukulia hatua za kisheria.
©Songea Municipal, Ruvuma.
HIVI PUNDE…
Thomas Chihongaki anasema, “Gaudansi Kapinga sio Mkazi wa
Kijiji cha Mbuyula bali hao Vijana walikuwa wageni kabisa hapo Kijijini mwenzie
Kakimbia,”.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako