December 27, 2017

SALAMU KUTOKA LUNDU, ZIWA NYASA

Nawasalimu enyi waungwana nikiwa nimeketi katika ngazi za Kanisa Katoliki ambalo lilijengwa mwaka 1946 ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kumalizwa vita vya dunia. Mahali hapa nilipatiwa daraja la Kipaimara.
Kinachoshangaza jengo hili limekuwa imara maradufu. Jengo hili halina mambo yenu ya #ExpansionJoints. Jengo la Kanisa hili lilijengwa na waafrika wakisimamiwa na Wamisionari wa Shirika la Benedictine Fathers la Kijerumani. Kwa mujibu wa historia rasmi iliyohifadhiwa hapa matofali ya jengo hili yalifyatulia kijiji cha Liweta na Lundu kutokana na udongo mzuri. Aidha, matofali hayo yalisafirishwa kwa Boti ya Stella Maris. 

Wasalaamu!
"Bruda" Markus Mpangala OSB
Lundu, Nyasa.
Disemba 20/2017.

MUHIMU; Salamu hizi ziliandikwa kabla ya tarehe ya leo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako