February 19, 2018

MAMBA AKATISHA UHAI WA MJASIRIAMALI NGINDO

NA THOMAS CHIHONGAKI
Majonzi na Simanzi Vimetawala katika Kijiji cha Lundo na Ngindo Kata ya Lipingo kutokana na tukio la dada yetu Neema Kalanje(25) kupoteza maisha kwa kushikwa na kuuliwa katika Mto Lwika uliopo Kijiji cha Lundo. 

Dada yetu amekutwa na umauti huo jana Saa 5 Asubuhi akiwa katika shughuli zake za ujasiriamali wa kuuza Dagaa Nyasa aliowanunua Ziwani Asubuhi na kwenda kuwauza katika Kitongoji cha Zambia katika Kijiji cha Ngindo.

Marehemu alipofika katika Kivuko cha Mto Lwika kuna dalaja dogo la Mbao akaamua kunawa Maji ghafla mamba akatokea na Kumkamata. Baadae Taarifa zilisambaa kijijini  kwa mayowe na hatimaye Wananchi wakakusanyika na kuanza kutafuta na kufanikiwa kuuona mwili wa Marehemu.

Eneo hilo ni hatari kwani mwaka 2015 palitokea ajali na kujeruhiwa kwa kijana Ignas Magic Kalenyula na kumuua Thomas Nkoma. Rai yangu kwa Halmashauri kupitia Idara ya Maliasili kuangalia uwezekano wa kuwasaka wanyama hao na kuwatokomeza kabisa.

Pia Idara ya Ujenzi Nyasa kutusaidia kujenga daraja la kudumu katika eneo hilo. Picha za tukio nii kwa hisani ya C.Ngwata Diwani wa Kata ya Lipingo (Chadema). Natoa pole zangu kwa Familia ya akina Kalanje na Mdogo wangu Elisha Magunga kwa kumpoteza Mke wake Mpendwa...
RIP Neema

No comments:

Post a Comment

Maoni yako