August 29, 2007

Furaha Ni Kitu Adimu

Wengi tunadhani furaha ni kumiliki magari,wanawake wazuri,wanaume wazuri,kazi nzuri,nguo nzuri n.k lakini hawataji hasa kwanini mtu ajisikie furaha.

Furaha si kitu cha kuuzwa ma kununuliwa kama peremende kamwe furaha hailazimishwi bali huja kama anayehiotaji yupo sawa na kweli anahitaji furaha.Furaha si kwenda kanisani kupayuka,kulia,kuogopa mungu atakufa hivyo,kuogopa vifo n.k lakini fauraha haiji kama hitaki kuwa na furaha yenyewe.

Tujiulize kwanini leo Bili Geti anaamua kusaidia watu wa hali chini ambao wanadai kuwa ni masikini wakati ana mapesa,magari,mke mzuri,kampuni za mitaji mikubwa n,k lakini ameamua kusaidia watu wengine.Baaada ya kujikombea feza hizo kwa faida yeye anaamua kutoa bure kwa wengine ingawa suluhisho la kuondokana na hali ngumu si kutoa feza na magari.

Amkeni acheni ujuha,furaha ni kitu ambacho kila mwanadamu anakitegemea kwa mwingine,huwezi kuwa na furaha bila wanadamu wengine,acha rushwa,ubinafsi wape nafasi wngine nao wakupe furaha ya maisha wala haihitaji kununua dawa za kupata furaha kama huko kwa akina joji kichaka wanavyofanya.Furaha ni kitu adimu sana hakiji kwa kutumia nguvu nyingi au mapesa.