August 20, 2007

Nikiwa mbali...

Ndiyo nikiwa mbali natafakari sana kuhusu eneo nililopo la LUNDU,nafikiria sana kuhusu kijiji changu.Nakumbuka mengi niliyofanya,burudani,utulivu,upendo na amani,porojo na kila kitu ilimradi siku zisonge mbele kwa furaha,kijijini hakuna msongamano,hakuna vurugu kama mijini yaani raha tupu.

Nikiwa mbali natafakari sana kuhusu kijiji hicho namna ninavyokipenda,nalitzama jua la mawio na machweo katika ziwa murua la Nyasa,ziwa lenye dhoruba kali kuliko yote ulimwenguni lakini likitulia utapenda ndio maana rafiki yangu Mark Wood wa Uingereza,hachoki kuja NYASA,hachoki kwasababu anapenda mandhari yake safiiiii.

Maji salama yasiyo na chumvi kama hilo bahari lenu la hindi,ufukwe haunuki kama huo wa kwenu wa hindi achilia mbali kuwa mchafu ovyo kabisa sijui wamekufa kibudu.

Karibuni sana Nyasa msiogope wageni tunawakaribisha dira yetu ni upendo na amani.
Karibuuuuuu

2 comments:

  1. inaonekana unakipenda sana kijiji chako naamii unahihisi kufa kama hujakiona lakini sijui unazungumza toka ro0honi au unaghushi tu mwanangu

    ReplyDelete
  2. unakiona kijiji chenu kama roho?duu unawazimu kweli ndugu yangu tena wazimu wa upendo endelea kupenda eneo lako maana wengine wamekimbilia mjini na unaonyesha unablogu ukiwa hukohuko bushi sasa kuna migahawa ya kompyuta nini?

    ReplyDelete

Maoni yako