January 19, 2008

Songea,Nyasa na Mambo ya mjini

Kama kuna kitu kinakufanya mtu uwaze basi ni kupambana na mazingira mapya,iwe ya kimaisha au namna unavyokabiliana na hali ya hewa n.k.Naam mnyasa leo nimeibukia mjini Songea na kujikuta nashangaa tu mazingira mazuri na watu wema wa kila rika lakini hii haiwezi kunifanya nione na mahala bora zaidi kuliko Nyasa yetu.Nimeibukia mji huu ili angalu nipate jambo jipya la kuwasimulia wanyasa wenzangu maana imekuwa kama hadithi fulani ambayo kila mmoja wetu angependa kuifahamu au siyo ndugu wasomaji.Songea ni makao makuu ya mkoa wa Ruvuma hivyo kwa wanyasa kama sisi ambao hupata nafasi ya kutembelea mji kama huu lazima tuwe na jipya la kuwaambia.Ngoja kwanza jana nilikuwa namshangaa sana askari wa barabarani kwani sijawahi kuwaona huko kwetu nyasa wala hatujuui lolote kuhusu askari hawa kwani twajivunia Meli zetu kwa usafiri lakini huku mjini kuna askari wa kuchunga barabara kama mchunga ng'ombe fulani.Lakini naomba kuwaheshimu lakini sijui kama wameacha Rushwa za daladala.Aaah mi sijiu lolote

No comments:

Post a Comment

Maoni yako