February 14, 2008

Ndesanjo kasikia Kilio toka nyasa na GoDaddy.com yake

Nilichanganyikiwa kidogo,yaani nilihisi kuvurugikiwa Medulla Oblangata kwa siku kadhaa kwani sikuamini na baadaye nikajipa majibu Mwalimu katoweka Darasani kulikoni?Nilipatwa na ghadhabu lakini wapi bwana Mwalimu ni mwalimu tu itabidi uwe mpole kama kobe,Nilifadhaika nikaandika ujumbe mwalimu vipi mbona darasa limetoweka?Sikujibiwa bwana,hapakuwa na majibu zaidi ya leo kushuhudia nimejibiwa kwa vitendo.Yaani we acha tu.Ni hivi Huyu Mwalimu wangu alipotea ghafla hata sikuelewa kwa nini lakini karejea sijui kaogopa nini au labda anadhani kila kinachopotea katika jamii ni ufisadi{samahani natania baba}.Ni chereko sana hapa nyasa leo kwani najivunia mwalimu wangu bwana halafu watu wananiona mjanja sana kwakuwa sijishughulishi na uvuvi bali kublogu hata kwa muda mfupi. lakini kuvua ndiyo zangu mnyasa mie.....nicheke nina mwanya?
hebu mtazame hapo kulia kwa blogu hii pameandikwa Ndesanjo Macha,kama hujui huyu ni baba wa teknolojia Tanzania nzima na huenda afrika yote ukibisha nenda Globalvoices.com soma uone mambo.
http://www.jikomboe.com/ kwa jina lenyewe tu anastahili kuitwa mwalimu.Heko baba biashara itakuja baadaye tupe faraja wanao kwanza na urafiki daima acha hiyo GoDaddy.com yako

No comments:

Post a Comment

Maoni yako