February 07, 2008

Wanyasa kwa Samaki huwatoi kabisa,.. Hata wakiwa Ughaibuni..

Nilijikuta najiuliza hivi hawa wanyasa bila samaki ingekuwaje?Basi ni hivi nimepata waraka kutoka Ughaibuni,yaani dadangu huyu huko Ughaibuni anakwambia anakumbuka Magege yakiwekwa chumvi na pilipili pembeni we acha kabisa..Lakini usishangae nimepataje hii habari kwani utajua kuwa nipo hapa nyasa.Jibu ni ndiyo lakini nimeibukia hapa Mbinga hapa kama kawaida kudandia maisha.Dada anakumbuka samaki wa ziwa nyasa yaani njozi zote mambo ya nyumbani.Wanyasa, hebu soma sehemu ya ujumbe huu "Nimevutiwa na Blogu yako,mimi mnyasa yaani nakumbuka nilipokuja mwaka jana mwezi novemba nilipewa magege na chumvi kisha na pilipili yaani acha nijichane we acha tu nyumbani bwana".Mtoto wa kinyasa utamjua tu si unaona alivyochambua aina ya samaki hao? yani anajua viungo vyake na bila shaka liapewa samaki wa kuchomwa.Ukitaka kujua yuko wapi hebu peruzu jiografia nchi ya Sweden ilipo ndipo utajua ninachokisema.Dada yupo ughaibuni lakini hajasahau nyumbani {Tanzania}anakuja kutembelea,Je wengine mpo?Lakini ndugu yangu Ndesanjo anatembelea sana Jeff na wenzake.Mwenzetu anakumbuka samaki lakini amesahau dagaa,kambale,ntaka,mandongo,mbasa,ngogo n.k ndiyo nyasa hiyo watu wanaselebuka kwa raha kama dada yetu anavyoselebuka toka ughaibuni na samaki wa nyasa. Wanyasa kwa samaki huwatoi kabisa....yaani mpaka ughaibuni?

2 comments:

  1. kazi nzuri,nyumbani ni nyumbani na ukisha zoea kula samaki basi huwezi kusahau

    ReplyDelete
  2. kwa kweli mmenikusha mbali sana maana nakumbuka sana samaki kuhuma kunyanja. wale samaki ni watamu sana kama vile mbasa, mbelele,mandongu, mang'ongu, mjangahali,ngorukoru,mbufu,mabogubogu,ntaka,kipindi kile cha kuvua tulikuwa tunakoka moto na kuchoma mihogo pamonga na homba au tuhika ni uwali kuhuma kunyuma tukimbii lidele ni uwali. najisikia raha sana nipatapo yale ya zamani ya kwenda kushika likungu na kwenda kuchuma uyoga kipindi cha mvua.

    ReplyDelete

Maoni yako