June 20, 2008

Afya Njema Nyasa

Nakumbuka kuna wakati jamaa mmoja aliwahi kunieleza kwamba mwili haujengwi kwa matofali,sikumwelewa shauri nilikuwa sipendi tabia yake ya kula vitu vingi bila ustaarabu.Basi nilipokutana na akina mama hawa nikasema......kama siyo kuishi nyasa nitaishi wapi?Wakacheka na kusema kama ninataka ndizi niseme.... Nikashangaa kwani nilikuwa nasifia nyasa wao wanasema nichukue ndizi.Mwingine akaongeza kwa kauli ileile ya yule jamaa kuwa mwili haujengwi kwa matofali.Nikaelewa,kisha nikapewa mkungu wa mmoja.Nikasema AFYA NJEMA NYASA.tukaagana nikiwa tayari nimewapiga picha hii.Imekukuna sana?Yaani mimi hunitoi hapo.... haya tuanze kushindana kula hizo ndizi..

4 comments:

 1. Hapa ndo ummenikumbusha mbali sana unajua mimi nimeishi Kijiji kimoja kinaitwa Matetereka kipo katika tarafa ya madaba ee bwana we kule kuna ndizi na hicho ndio kilikuwa chakula changu yaani ni kubadili tu kuchemsha, kukaanga, kuchoma au mbivu. Halafu pia nimekumbuka makazi yangu yaani pale nipozaliwa Lundo yaani nyumba nzima ilikuwa imezungukwa na ndizi. Nakuomba au niseme naangiza mkungu mmoja wa kaporota. Yaani nimetamani kama niwapokee (kuwatua) na kuanza kula sawa mimi niko katiaka hilo shindano la kula ndizi tuone....

  ReplyDelete
 2. markus mpangala22 June, 2008

  Ndugu yangu kwa kweli hongera kwa kukumbuka nyumbani,kukumbuka mahali ulipowahi kuishi. maana toka hapo hadi huko ughaibuni hakika ni kumbukumbu nzuri na muhimu katika maisha kwani inakupa uelekeo wa maisha ya kila siku.Najua unakumbuka mengi sana ndiyo maana hata unatamani kuwatua....lakini usijali uatakula tena kwa raha zako karibu tena nyasaa......

  ReplyDelete
 3. asante sana, si nimekuambia nafunga mizigo sasa.

  ReplyDelete
 4. Inaonekana Mbinga kuna kila aina ya resource, hivi ndizi za mbinga huuzwa wapi na kuna capacity kiasi gani, yaani nikitaka kuwekeza let say ekari 100 za kilimo cha ndizi naweza kupata hiyo ardhi?
  Kweli Tanzania hatustahili kuwa maskini?

  Mungu ibariki Tanzania

  ReplyDelete

Maoni yako