June 22, 2008

Eti Huo Ni Unyanyasaji Kwa Wanawake...?

Mimi sijui ndiyo maana nimeuliza wanazuoni mnisadie kwani hapa nyasa naona ni hali ya kawaida mwanamke kubeba mzigo wa kuni kama huu.Pengine wenzetu mnaweza kujua nini maana ya unyanyasaji kwani kwetu nyasa tunasikia tu kitu kama hicho lakini hatukijui tunaomba kufunzwa.Huyu mama kabeba kuni{HANJU}kwa ajili ya shughuli za nyumbani n.k Je huo ni unyanyasaji kwa wanawake?mjadala....

4 comments:

  1. Anonymous22 June, 2008

    unyanyasaji labda neno mbaya, ila ingependeza kama akina baba nao wangekuwa wanawasaidia akina mama. Lakini kwa sasa inaonekana ni kama mila/desturi au niseme ni kazi ya akina mama je nani anasema hivi sijui je ni kazi gani ni kazi ya akina baba kwani ukiangalia akina mama wanakazi nyingi mmo kuzaa watoto, kuwalea, kujua leo na siku zijazo watakula nini kuchota maji, kusafisha nyumba, kuokota kuni na kisha kupika chakula. hapo sijasema kazi zote kwani nawaachia na wenzangu pia.....wasema si mjadala karibuni (...)

    ReplyDelete
  2. Mimi naona ni unyanyasaji tu pale mwanamke anapokuwa anafanya kazi zote huku mwanaume anashinda kilabu cha pombe kuutwika na akirudi nyumbani anataka chakula na mapenzi wakati kazi hasaidii.
    Huko vijijini hali ni mbaya sana, wanawake wanateseka sana na wamefika mahali wanashindwa wafanye vipi.
    Wanaume tunahitaji kubadilika na kuwasaidia wake zetu kazi mbalimbali za familia, kama kuni, kilimo, ufugaji, watoto kuwapeleka vituo vya afya, na pia kuwapenda wake zetu wajisikia kweli kuwa katika ndoa ni raha.
    Kuna mila na desturi ambazo zimepitwa na wakati na inabidi zitokomezwe ni mimi na wewe tunatakiwa kufanya haya kwa vitendo si kuongea tu.

    Bila mwanamke, mwanaume mashakani.

    Upendo daima
    LM

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na mwanchi iliyetangulia ni lazima tufanye kitu kuwaokoa wanawake wa vijijini. Amini bila mwanamke nyumba si nyumba

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

Maoni yako