June 12, 2008

Mnyasa,Mwanakijiji na Markus X

Kuna tofauti kubwa kati ya wivu na usongo,vivyo hivyo wivu humuua mtu mjinga,na huwezi kumchukia mtu unayemuona halafu ukampenda mungu usiyemuona yani itachekesha sana.Unajua kwanini?Kuna jamaa anapenda sana kupongezwa basi jana nikamwambia haniwezi mimi mtoto wa kijijini,mnyasa na mwana wa Malcom X.kilichofuata ni kicheko,halafu akagundua kuwa nimekasirika kisa kabeza majina yangu,nikasema hana jipya mimi ni mwanakijiji,myasa mpaka kufa halafu nikaongeza Markus X.Ndiyo mimi ni mnyasa wala hilo halina ubishi,kwani hiyo ni fahari yangu wala haina maneno.Pili Mwanakijiji,ni kweli kwani mimi nimezaliwa kijijini Lundu hivyo napenda kuitwa Mwanakijiji yaani toka huko nyasa kwenyewe.Sasa unajua kisa cha kujiita Markus X?Nimeamua kujita hivyo labda nitaridhika maana kila ninapoona sura yake Malcom X na kusoma hoja zake basi nahisi navaa ushujaa na ukombozi wa watu wa nyasa lakini sina maana kwamba wanamatatizo bali napenda nikimaliza ujuzi wangu ninaoutafuta sasa nataka nikawe mwenyekiti wa kijiji chetu cha Lundu.Napenda falsafa za Malcom X mpaka napata wazimu{natania usije ukadhani kichaa kweli}.Ni kweli nimeamua kujiita Markus X ili mjue kwamba nina utajiri wa akili lakini nimekuwa fukara wa kipato lakini ni mimi Markus X,Mwanakijiji na Mnyasa asilia.

2 comments:

  1. kwanza nilitaka kusema umechanganyikiwa, lakini baada ya kufikiri kwa makini nakubaliana nawe kwa sababu Nyasa LUNDU itakuwa na mwenyekiti mzuri, mwenye elimu ya kutosha na ajuaye nini anaongoza. Pia nimegundua jinsi unavyoipenda NYASA yako(yetu) nakutakia mafanikia mema pia nawaonea wananchi wa Lundu WIVU hapo baadaye kukupata wewe kama Mwenyekiti.

    ReplyDelete
  2. markus mpangala22 June, 2008

    Nadhani niatkuwa mwanakijiji mwema na kufanya kazi kwa bidii sana.Kisha kuwaalika wale ndugu zangu wa Malawi waje wafurahie matundaya wanyasa wenzao au siyo wanyasa wenzangu

    ReplyDelete

Maoni yako