June 10, 2008

TANGAZO; Nafasi Ya Kazi Nyasa

Kuna nafasi ya kazi hapa nyasa.Ni kazi nzuriikiwa unasifa hakuna haja ya kulemaa njoo haraka.Hakuna masharti magumu bali ni afya njema isiwe na migogoro.Kazi yenyewe ni kuwa TARISHI kwani wanyasa tunampango wa kuwatumia samaki na vyakula vya nyasa kwa wote wazaliwa wa nyasa waliopo mbali hususani wale wa ughaibuni.Msingi wa kazi yenyewe ni kwamba tunataka kutuma vyakula vya huku nyasa kwani tumeona ndugu yetu hapati samaki kwa uhakika.Pale Ruhuwiko kuna hamu ya vyakula vya nyasa hivyo usipoteze nafasi hii kwani malipo ni kujitolea wala hakuna sumuni au shilingi bali ni moyo wa upendo.Kama unataka kazi hiyo tuma wasifu wako ukiambatana na uzoefu wako wa vyakula vya nyasa na uwezo wa kufanya kazi.Tazama mfano wa vyakula vya nyasa hapo juu

1 comment:

  1. Anonymous10 June, 2008

    Mimi ni msichana,jina langu ni Agnes Mapunda na nina umri wa miaka 28.Nimeona tangazo la kazi na ninatuma maombi kuwa nina uweza wa kufanya kazi hiyo pia nina uzoefu mzuri wa vyakula vya aina hii. ukitaka ninaweza kuambatanisha na cheti changu.

    ReplyDelete

Maoni yako