June 13, 2008

Ile Nafasi Ya Kazi Imepata Mwenyewe..

Unakumbuka lile tangazo la nafasi ya kazi hapa nyasa?Lisome.Ingawa sikupata ruhusa ya kumtangaza lakini huu ndiyo ukweli kwamba ile kazi imempata mwenye ujuzi wa kutosha kwani vielelezo alivyonavyo hakukuwa na haja ya kungojea wengine.Lakini pamoja na wale wasiochaguliwa katika nafasi hiyo tunaomba wasisite kuomba tena pindi watakapoona tangazo lingine la kazi kwani tunahitaji wafanyakazi wengi.Kwani nafasi hii ni ya juu zaidi na mshindi wetu anavigezo na utaalamu wa hali juu hivyo jamani...pigeni makofi tafadhali....eeh makofi tafadhali....aaahaa samahani siyo kutwangana makofi bali ni kushangilia kwa pongezi kwa mshindi wetu.Jina lake ni......naomba uje hapa mbele ujitambulishe mwenyewe......makofi tafadhali.......makofi....makofi....makofi tafadhali....

2 comments:

  1. Anonymous13 June, 2008

    Eeh jamani dada huyo ana bahati kwenda kufanya kazi nyasa. Mimi ndo kwanza nilikuwa mbioni kutuma maombi yangu kweli chelewa chelewa .....kama waswahili wasemavyo. Basi bwana hii ndo dunia kwa hiyo nitakuwa macho hapo maombi mengine yatakapotoka. Hongera sana dada yangu. Pia nakutakia kazi njema sana.

    ReplyDelete
  2. markus mpngala22 June, 2008

    Asntekwa pongezi nampelekea wala usikonde.Hapa nilikuwa nawasiliana naye,lakini kidogo alipata homa hata hivyo mudamfupi ujao atakuwa kazini kwani nimemuamini sana na anapenda kazi yake

    ReplyDelete

Maoni yako