July 03, 2008

Bandarini Mbamba Bay Utamu Kolea

Hapa ndipo Mv Songea inapotia nanga.Tazama kwa umakini ujione uzuri hata kama ni kidogo acha tujivunie.Unajua nini?Kuna jamaa anapenda sana kuja hapa kutazama shughuli zinavyokwenda.Mara kwa mara ukimuuliza anakwamba anaenda kumpumzika Bandarini kutazama kazi na vituko vya wanyasa visivyo na shari.Mv Iringa nayo hutia nanga hapa ila lile meli la Malawi kubwa kama nini sijui linabaki kilindini na kutumia maboti.Jamani meli kubwa hilo utafikiri za wale jamaa walioenda kuvamia uarabuni.

2 comments:

  1. Nadhani hata mimi ningemuunga huyo jamaa mkono kwenda hapo bandarini na kupunga upepo

    ReplyDelete
  2. kaka Markus hujatupatia yaliyojiri kwenye kikao cha wanyasa kuchangia maendeleo ambayo hawajachambua mahitaji yake...

    ReplyDelete

Maoni yako