July 02, 2008

Karibuni Tena Mbamba Bay

Ukitazama mbele kabisa unaona kama kuna majengo fulani-hapo ni karibu na Hoteli ya Neema.Yaani mahali pale ni pazuri sana kuna barabara toka uwanja wa hoteli hiyo mpaka ziwani yaani unabarizi tu taratibu siyo kwa usafiri bali matembezi.Kwa wapendanao wanajua matembezi lakini mnyasa hata sijui mimi kuvua samaki tu.Hili eneo lenye mawe pana uwazi mzurisana ambao hutumika kwa kujipumzisha nyakati za mchana.Hii ndiyo Mbamba Bay ndugu yangu karibu tena mmm lakini dadangu pale Ruhuwiko bloguni anaumia shauri amekosa sana utamu wa nyasa....ngoja nitakutumia basi la ungo uje kwa kasi kisha kurejea ughaibuni.

3 comments:

  1. Anonymous02 July, 2008

    Ic,

    Yaani naamini nikija mbinga, siwezi kurudi kwani kuna kila aina ya vivutio, halafu hayo majengo kwa mbali mbona sioni nahisi macho yangu yanahitaji lensi.

    Naomba msaada wako je ni miti aina gani inastawi huko mbinga, je kuna pines? ni miti gani ni hardwood? na miti ipi ni soft wood, je unaweza kuniwekea picha zake. Na je, mbao nyingi mnazotumia katika ujenzi na shughuli za kila siku ni za aina gani, je zinazalishwa hapo Mbinga au kutoka sehemu zingine kama Njombe nk.
    Natanguliza shukurani zangu kwa kazi nzuri.

    Lazarus Mbilinyi
    Canada

    ReplyDelete
  2. Anonymous02 July, 2008

    Ni kwamba pale pembezoni mwa mlima kuna majengo sema tu kwamba picha imejibana sana.Pale pana eneo la hoteli nzuri sana.Naomba mnisamehe kwa kutoonekana vyema kwani mbali sana.Mle pembebi-pani na eneo lote linaitwa mtaa wa zambia

    ReplyDelete
  3. Anonymous03 July, 2008

    Asante sana,

    Inaonekana Tanzania kuna mitaa mingi sana inaitwa mitaa ya Zambia, hata Makete kuna mtaa unaitwa mtaa wa Zambia nihisi na Tunduma kutakuwa na mtaa wa Zambia

    ReplyDelete

Maoni yako