July 07, 2008

Mahaba Ni Raha na Faraja.....

Kuna raha,utamu,faraja,nidhamu na ukakasi.Au kuna ile hali ya kuona kwamba unaishi halafu hufurahii maisha yenyewe,unabisha?...Jamani samahani usije ukadhani kwamba nimechanganyikiwa.Lakini mahaba,raha na mafunzo ya kuyasaka yapo. hakika.Unajua kwanini.Nakumbuka wakati fulani nikiwa hapa nyasa maisha yanakwenda chini ya amri za wazazi{jambo ambalo hadi sasa nafuata amri za wazazi hao} lakini huku pembeni unastawisha gumzo,watu wanafurahia wanaona gumzo limenawiri utafikiri limewekwa mbolea kumbe mnyasa anaongoza gumzo.Gumzo lenyewe nimelikumbuka wakati ule tunatafuta ujiko mitaani si unajua mambo ya kinyasa?Basi hayo mahaba tunawaona watu yameshamiri ni raha tupu,kila mtu anaona hii ni raha na faraja.Kuona hivyo jamani mbona sisi hatuna gumzo la kustawisha mahaba na raha.Jamaa akaibuka kwamba inawezekana katika nafsi zetu hakuna maana ya mahaba..lakini tukamuuliza tutafute vipi?Eeeh jamaa akaanza ukitaka mahaba lazima uyatafute hakika hivi au ukitegemea kuwa yanakuja hilo umekosea.Basi suala lenyewe ni hili kuna rafiki yangu mnyasa hapa ana mambo ya ajabu kila siku yeye analalamikia kukosa mahaba na faraja za mahaba yenyewe.Kumbe nimegundua anaogopa kutafuta,akiona akina dada anatamani kuyasaka mahaba lakini anaogopa kuanza hata kuongea neno japo kusalimia...lakini ananilazimisha nimfundishe kuyatafuta mahaba shauri ni faraja.Nimeshindwa sababu mimi nimezoea kuvua na kutengeneza nyavu zangu shauri yake....jamani anayeweza popote ulimwenguni amsaidie au awasiliane nami hapa bloguni nimsaidie lakini tafadhali hakikasha unaweza kumtimizia maana ameniambia kuna zawadi nono kwa atakayemfundisha kuyasaka...au labda ajifunze katika blogu ya kaka Mbilinyi...ngoja nitamwambia ili anipunguzie mzigo kwani nimechoka kelele zake...lakini rafiki yangu mmmhh siwezi kuacha kumsaidia....ngoja nikomee hapa kwanza..

2 comments:

  1. Anonymous08 July, 2008

    Kwanza kabisa inaonekana kama ulivyosema ya kwamba huyo rafiki yako anaogopa hata kusalia akiwaona akina dada. mmmh itakuwa ngumu kwa yeye kutafuta raha, faraja pia mahaba. Je? umemuuliza kwa nini anaogopa akina dada na je? anaogopa kina kaka pia nikijua hili labda itakua rahisi kumshauri

    ReplyDelete
  2. Anonymous08 July, 2008

    huyu jamaa napenda sana utani na anaongea vizuri na akina kaka ingawa kwa wale aliowazoea tu,yaani kama mtu hajamzoea anakuwa mpole kama maji ya mtungini lakini ngoja nimejaribu kuongea nae.Ila sasa naona anajaribu kujisahihisha...lakini nimemtahadharisha awe makini na akina dada wa siku hizi maisha yao siku stini kama mahindi ya masika...natania

    ReplyDelete

Maoni yako