July 05, 2008

Muwe Makini Usafiri wa Meli Mwezi Julai

Nimekwisha kusema kwamba mwezi Julai kuna dhoruba sana hivyo kama siyo wazoefu wa kusafiri kutumia meli basi nashauri kuacha.Wakati huu dhoruba kali watu wanatapika hovyo,hali ya hewa mbovu yaani mawimbi sana.Huu ni msimu wa dhoruba toka julai mpaka mwezi agosti mwishoni inategemea mabadiliko ya hali ya hewa maana inaweza kupitiliza hadi Septemba.Kuweni makini au tumieni usafiri wa magari toka Ng'ombo,Mbamba Bay,Liuli na mwambo wotewa ziwa nyasa usafiri upo Lundu, Lituhi na maeneo mengine

1 comment:

  1. Anonymous06 July, 2008

    Ndugu yangu sasa hivi ni balaa sana kwani wimbi linapiga kila upande.Acha kabisa na wale wasiozoea shauri yao wakikupuuza......yaani watajiju na kujjiua pamoja

    ReplyDelete

Maoni yako