September 27, 2008

SONGEA LEO HII ; Afungwa maisha kwa kulawiti

IMEANDIKWA NA HAPPY KULANGA,
SONGEA


Mkazi wa kijiji cha Mageuzi Mlilayoyo wilayani Songea Vijijini bwana Maneno Katuna(24) amehukumiwa kifundo na mahakama ya wilaya ya Songea baada ya kukiri kosa la kumlawiti mtoto wa darasa la kwanza wa shule ya msingi Mageuzi mwenye umri wa miaka 8. Mwendesha mashtka Inspekta Patrius Mlowe alieleza mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Joseph Emmanuel Foyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Septemba 16 mwaka huu asubuhi kwa kumlaghai mtoto huyo kuwa anataka kumpa Chai. Aliiambia mahakama kuwa baada ya mtoto huyo kuingia ndani alimvua nguo na kuanza kumwingilia kinyume na maumbile na kumsababishia maumivu makali hata akshindwa kutembea. Alisema mtoto huyo aligundulika na wasamaria waliokuwa wakipita jirani na nyumba hiyo walimwona mtoto huyo akilalamika kutokana na maumivu makali aliyokuwa ameyapata. Mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka lake alikiri kosa na kuiomba mahakama imsaidie kwa maelezo kuwa umri wake kuwa mdogo na anahitajika katika ujenzi wa taifa. Hata hivyo madai yake yalitupiliwa mbali na hakimu Fovo ambaye aliamua kumhukumu kwenda jela maisha yake yote,akisema adhabu hiyo ni fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

1 comment:

  1. Ama kweli dunia imeharibika kiasi hiki tumbo linaniuma ninaposikia habari kama hizi yaani sasa mpaka Songea yetu. Hii ni tabia ya unyama kabisa huyu mtu lazima ni kichaa, kwanza ilibidi anyongwe kabisa kifungo cha maisha, sawa lakini amempa binti ya watu ndoto mbaya ambayo hataisahau maisha yake. Pole sana mtoto kwa maumivu makali pia wazazi.

    ReplyDelete

Maoni yako