November 17, 2008

kuvua dagaa usiku


dagaa wa ziwa nyasa ni watamu sana, wananoga mno, ukila unajiumauma tu hamu na kuzidi kunogea. SASA ukitazama picha hii utaona KARABAI zimefungwa mtumbwini, hapo ndipo kazi inafanyika kwani ukisha funga hivyo kazi inaanza kwenda kilindini na anyavu ya kuvulia kusaka kitoweo kunoga na utamu kuliko chochote..... ebu taja kitu kingine kitamu kuliko dagaa? najua utataja nanii....... nini ile ...... sijui ebu inaitwaje!!!! aahaa tuache, hayo. haya ndiyo mambo ya nyasa na zana zao

4 comments:

  1. Eeh, bwana we usinikumbushe na usiniambie yaani hao dagaa wakisha fika nyumbani halafu wanatengenezwa unawapanga kwenye chungu au sufuria na wanaiva polepole(lighanda) rafiki yangu hapo lazima ugali uwe mkubwa sana la sivyo itakuwa vita. Nyasa bwana raha sana GWALI NA SIPA kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  2. yaani LITONGE linakuwa likuwa kubwa halafu unatengeneza kama kisima pale katikati na kuteka mchuzi weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee mpka akili inasema uko wapi kaka SIMON KITURURU mzee wa MAWAZONI raha hii jamani huku nyasa. mm najua napenda sana BIA ha ha ha ha MZEE WA CHANGAMOTO karibu sana nyasa tena sana

    ReplyDelete
  3. Nikianza kujibu swali ni kuwa kama kuna kitu kitamu kuliko Dagaa wa Nyasa basi ni "dagaa waliokomaa" (samaki). Ama mnaonaje? Lakini utamu wa dagaa na hata mboga ya aina yoyote vuategemea upishi. Mimi najitambua kuwa mtaalamu wa mapishi na ndio maana naweza kukupikia Mchicha ukanoga kama dagaa na dagaa waka-taste kama kisamvu. Lol
    Ila habari ya uvuvi kwa hakika ni shughuli pevu na nasikitika kuwa pamoja na kuleta ladha na afya kwa jamii zetu, bado wavuvi wanaishi maisha ya chini na uwezeshwaji wa kazi zao ni mdogo sana.
    Ni CHANGAMOTO YETU sisi tunapotafuna na kufurahia ladha ya dagaa kukumbuka yale wanayopitia wavuvi usiku kucha kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya "minyoo" yetu. Kama hatuna cha kuwa, basi TUWAOMBEE SALAMA huko wafanyapo kazi.
    Tuonane "next ijayo"

    ReplyDelete
  4. @Markus: Huko lazima tuje tu angalau na togwa!:-)

    ReplyDelete

Maoni yako