August 15, 2009

YASINTA NGONYANI NA JOHARI YA MATUMAINI

Nafungua anuani pepe nakuta ujumbe, najiuliza kulikoni ni nani huyu? Alaah kumbe mwana wa nyasa, aliye ughaibuni? Ni mwanzo wa kumbukumbu, furaha na burudani. Mzaha wa hapa na pale kustawisha gumzo. Mtandaoni kwa saa nyingi mazungumzo yasokwisha hamu? Hatimaye ndiyo huyu tupo uso kwa uso tunazungumza tunapiga gumzo hapa na pale najiuliza maswali kadhaa kuhusu huyu mtu lakini najua ni mungu ajuaye mengi.

Mawazo yangu yaavaa uhodari wa kujua na kutaka kuona kile ninachoamini. Siku zinapiga miezi, mwaka na saa zote. Nipo ghorofa ya pili, nasoma ghafla ujumbe mfupi unaingia katika simu, salamu toka ughaibuni, najiuliza nitende vipi kwa mwandada huyu? nafunika vitabu na daftari, namtazama mwenzangu pembeni ananikodolea macho anashangaa vipi naacha kusoma halafu nachezea simu? Namweleza kuna jambo, nataka kuongea na mtu kwanza.
Tayari tunajadili hili na lile najadili mambo kadhaa yenye maudhui ya nyasa, halafu tunakumbushana mambo ya Lundo na maisha kwa ujumla.

Inawezekana usinielewe msomaji wangu mpendwa, lakini mantiki yangu ni kukupa mwanzo wa YASINTA NGONYANI na MARKUS MPANGALA. Ni kama andiko la wakristo la yesu alivyowaambia msihangaike kwa lolote wala msibebe vyakula bali mwendako mtajaziwa. YASINTA ni kiumbe mwenye sifa ambazo kila siku naziwazia, najaribu kutafakari, nakumbuka stori zetu za hapa na pale, nakumbuka yale mambo ya WAOOOOOOOOOOO!!!!1 Hee kumbe hatuko peke yetu, tunatulia na kutafakari, tunaleta mzaha kidogo na kustawisha gumzo, mambo ya hapa na pale. Usisahau tupo umbali wa maili nyingi lakini ikawa dakika kuwepo ana kwa ana.

Mimi sinywi soda, situmii pafyumu, wala mafuta makali, siweki dawa nywele zangu daima ni rasta. Nauliza swali aaaahh ndiyo maana Erick naye anapenda sana Rasta siyo? Kicheko kidogo..., namtazama kwa shauku ya kujua mengi....LAKINI nagundua kama kile alichosema Koero kuwa YASINTA NGONYANI ni binti wa kitanzania. Sifa moja kubwa aliyonayo ni MAZOEZI na ukimtazama ni unaweza kubabaika ukasema umri wake ni 23 au 26 hivi kumbe huyooooo.

Hapa nyumbani nina bustani ya matunda na mambo mengi ya nyumbani wala siwezi kubabaikia hayo mambo ya wazungu. Mi hee unaweza kudhani mtu unayezungumza naye anatania lakini kukweli ni binti mwenye itikadi msimamo mkali. Nakumbuka nipo Mbeya, nikabandikwa maaswali lukuki, stori nyingi lakini kikubwa ni faraja za hapa na pale.
Msomaji wangu, huyu Yasinta nina mengi ya kumwelezea lakini nafupisha na kutoa vipande ili upate msingi kamili. Hata hivyo nimemlazimisha kucheza muziki wa KWAITO anacheza usipime kabisaa, majuzi nikamwambia ebu selebuka na MYEKE BABA ya Mandoza... akacheka kidogo.

Nikumbushe msomaji YASINTA ni mkarimu, mtulivu, mkali, mwenye upendo, smikivu, mdadisi ndiyo maana nilimwita Mama Maswali magumu, mchokonozi. Nakumbuka kuna kitu alinichokonoa lakini nikajua udadisi ukaanza.... tusijali hayo lakini nakwambia kama huwezi kuishi na YASINTA basi wewe ni kiumbe wa ajabu. Mara nyingi utamsikia Markus mdogo wangu unatakiwa kujali muda wa kupumzika, utulivu na kujenga afya kwa kufanya mazoezi....
Wakati mwingine inakuwa kama unaota kulala gizani na kulamba mchanga halafu huchafuki kumbe upo ukwelini na unawaza ukweli uleule wa siku zote.

Sikiliza mimi nataka kufanya kitu fulani katika blogu, nifanyeje? Ahh tunachapa gumzo tunafundishana haya na yale. Na fundsho letu kuu la mwisho lilikuwa pale ufkweni kuhusu NeoCounter. Ni mambo matamu ya teknolojia.
SWALI UNAJUA ALIANZAJE KUBLOGU NA KUIJUA BLOGU YA KARIBUNI NYASA?
Kuna kisa cha YASINTA katika blogu yangu hii ambayo naomba msomaji ukitafute. na mara nyingi amenihimiza kuandika tena kwani amevutiwa nacho.
Kumbe kuna siku alikuwa akitafuta akina YASINTA wenzake wapo wangapi duniani, .... ndiyo hapo akutana na KARIBUNI NYASA na kisa kile cha Yasinta mwenzake. vilevile nilimpatia kazi ya kuchoma samaki kama unakumbuka msomaji kuna TANGAZO LA KAZI NYASA, yeye ndiye alishinda. Ila anapenda sana kula MAEMBE halafu na tabia yake ya KUNYWA CHAI ISIYO NA SUKARI yaani CHINGAMBU ni moja ya vionjo vyake na ambavyo nakiri ni MTANZANIA.
Nikamwambia niseme au nisiseme kile kitu fulani....... aaaah Msomaji wangu utanichoka nadhani unaweza kudhani nafanya mzaha. Lakini kiini chake ujue tu ni binti ambaye naona tofauti yake na wengine ni mtazamo na misimamo yake isiyotetereka. Ni mdadisi sana huyu kiumbe, hachoki kujifunza kila mara lakini ndoto yake ilikuwa SISTA yaani wale watawa... utakumbuka ndoto yangu ilikuwa kuwa Padre lakini yamepita...SAHAU. Nakumbuka nikawa namlazimisha kumsoma kaka Ansbert Ngurumo....

Upendo wake na namna anavyoweza kujadili na watu ni kitu ambacho kinanifanya wakati mwingine nimwambie nina wivu sana, na hilo sifichi na nimesema daima ana anajua hilo. Mungu kamleta kwa kusudio la kupendwa na watu wala hana mengi. JE UNATAKA NIKUWEKEE PICHA TULIZOPIGA? aaaaaaahh msomaji nadhani hii stori ndogondogo ni habari kamili ingawaje imekaa mshazari. mtanisamehe kwa kutoweka picha tulizopiga.....
Watoto wake anawaeleza kabisaaa..... nakumbuka anasema na Camilla.... mwanangu funga kanga , lazima kutii utamaduni wetu sawa? Camilla huyoooo anatoka ndani ya bwawa... anaiendea kanga.... mrembo huyu anachukua na kuifunga mwendo wake wa maringo taratibuuu kama twiga najongea mezani. Pembeni Erick sijui kiswidi chao wanasema Irik au? Kijana mpenda mazoezi kama mamake... anafuga rasta.... lakini siku hizi kazinyoa bwana...... a ha ha ha ha!

YASINTA GERVAS NGONYANI.... ngoja nikutaji jina leke jingine..... aaaah hapana siyo ruksa ni mimi tu nalijua au vipi usitake kujua sana. Ni kweli Yasinta mpenzi wa lugha ya nyumbani na bahati nzuri ni mtundu wa kujua lugha za wengine, najua ni wachache wanamudu hilo... lakini ameweza kujifunza lugha za wanyasa wale wanaongea kama wamalawi.... zile MULIBWANJI.... halafu tunahamia mazungumzo katika kimatengo... kingoni chenyewe, kimanda, kimpoto.... kinyakyusa..... nk. ukitaka kufanikiwa maishani ni lazima ujue utamaduni wako na kuheshima na utajua wapi unatoka.....
YAKO MENGIIIIII SAANAAAAAAA............................... tutahabarishana siku nyingine.... manake kuna siri, mafanikio, shubiri na mwenendo mzima wa maisha yake.... harakati zake........ NITAKUMEGEA MAMBO MSOMAJI WANGU, na usisahau kumsoma pale kwa dada Koero( huyu naye subiri simulzi zake nimekuandalia ndugu msomaji na nitajibu maswali ya wanablogu fulani walioniuliza kuhusu YASINTA na hata huyu Koero) sawa? we tulia tuuuuuu
Mwisho wa juma mwema!!!

6 comments:

  1. Huyu Yasinta yupo juu. Alianza kaka Bwaya kutaka da Yasinta ajielezee. Binti wa Kingoni akamwaga sera.

    Akaja da Koero. Akamwaga sifa tele.

    Leo mshikaji wetu mwanaharakati Markus kammwagia sifa tele.

    Sasa mimi ntaongea nini? Ntaharibu mchuzi wajameni. Huyu Yasinta ni kweli anastahili hivyo.

    Lakini, swali la kizushi kwako da Yasinta, hivi huoni makada tunavyokumwagia masifa kede kede? Hebu fanya fanya mwakani uje, ubunge ubunge, ubunge huko Peramiho.

    Wapiga debe tupo!

    ReplyDelete
  2. Mmm hata mie najiuliza hivi huyu Yasinta ni kiumbe wa kawaida kweli au mbona ana sifa kede kede. Ila Yasinta unastahili hizo sifa. Shukrani Markus kwa kuweka hii mada hapa leo.

    ReplyDelete
  3. Wow! Sina la kusema zaidi ya AHSANTE SANA Markus maana nimekuwa bubu kusema zaidi nashindwa

    ReplyDelete
  4. MARKUS, AHADI NI DENI, NASUBIRI SIMULIZI ZA DADA KOERO HAPA KIBARAZANI KWAKO,,,,,KWANI TWATAKA KUJUA MENGI JUU YA MLIMBWENDE HUYU

    ReplyDelete
  5. VYOTE WATAIGA LAKINI SIYO KIPAJI CHA YASINTA.
    -----------------------------------------------
    R.Njau

    ReplyDelete

Maoni yako