November 17, 2009

FIKIRIA SANA, USIAMINI SANA, AMUA WEWE

Mara ngapi umesoma kitabu au mahali ambapo panakupatia jawabu ambalo linaleta ukakasi kwako? Unaweza kufikiria lakini kama huwezi kufikiria basi jaribu kunisoma halafu fikiria kisha jipe jawabu kamili uone ukweli ulivyo.

1. Usiwe mwadilifu kupita kiasi unaweza kuwa mkiwa bureee maana mungu mwenyewe inadaiwa alisema hilo. Na kwakuwa kuna watu wanaamini kuwa dini za ukristo na Uislamu ni mwisho wa yote, hawajipi muda kuhoji, kwanini dini hizo za jamaa kutoka mashariki ya kati ambapo mmoja alikuwa akivaa misalaba mikubwa na mwingine alikuwa akifuga ndevu na kupka hina. Mbona kuna Wabudha, wahindu n.k angalia usiwe mwadilifu kupita kiasi.

2. Usiamini kitu chochote kwasababu tu kinasemwa na mtu mwenye busara. Pima mambo yako ewe mwanadamu usikubali tu kama ilivyo ndivyo bali unavyoamini ndivyo.

3.Usiamini kitu chochote kwasababu tu watu wengi wanaamini. Ndiyo maana sitaki kusikia dini ambazo zimejaa vimelea bya kutohojiwa, ambazo zinasadikisha ati ilikuwa lazima watakao hoji na wapingaji ukristo. Nimelelewa katika msingi wa dini zenyewe lakini ninachokiona katika ulimwengu wenyewe nashangaa tu. Kwani lile sanamu la mwanamke aliyepanda mnyama aliyepo pale nje ya bunge la ulaya ni nini kama siyo ushetani kwa mujibu wa UFUNUO WA YOHANA? soma tuulewe vema. Si mnadanganya na dini zenu kuwa Obama alikosea kuapishwa? wadanganyeni haohao ili mnyasa nisalie kuamini vile ambavyo naamini.

4.Usiamini kitu chcochote kwasababu tu vitabu vya kale vimeadnika. Yako mengi tu, mbona tunadanganywa Nostrodamus alitabiri vita vya dunia vya 3, alitabiri kuzaliwa kwa Adolfu Hitler na mengine mengi kama mapinduzi ya Ufaransa....lakini hatusemi kuhusu Mysters School ya Freemasons ambazo zilimfindisha kufundisha ushetani wake.

5 Usiamini jambo lolote kwasababu tu vitabu vitakatifu vimeandika. Hapo mie simo lakini unaamini kuwa simulizi za mambu wa mashariki ya kati ni chanzo cha kuwepo wa sisi. Alaah kumbe ilikuwaje aliyeletwa kwaajili ya Babeli na wayahudi akawa wa dunia nzima? Na historia ya Roma inaweza kunisadikisha kwamba niamini ndivyo ilivyo nisadiki tu bila kuhoji? Niamini anayekupiga kwenzi akuchape na mitama?

6. Amini jambo kwasababu wewe mwenyewe umelipima na ukaliona liko sahihi.

Ndiyo maana nasimimia hoja kwamba sihitaji kanisa wala msikiti wowote, sihitaji mchungaji wala ninachokiandika sikitumikii nakitumikia tangu mwaka 1996 hadi leo hii. Je unafikiri dini yako ni bora kuliko ya mwenzio? Unafikiria kanisa lako ni bora kuliko la mwenzio? Unafikiri sadaka yako ni bora kuliko ya mwenzio?

No comments:

Post a Comment

Maoni yako