November 15, 2009

HIVI PUNDE:.....kikao cha NYAZODE kimemalizika

Baada ya kutoka likizo mara vyuo vilipofungwa kwa muhula wa kwanza kumaliza. Na sasa kukiwa kumeshaanza muhuala mwingine hatukupata muda wa kuongea wala kujadili kwa kina kuhusu mradi wetu wa NYAZODE. Lakini leo hii jumapili HIVI PUNDE kumemalizika kikao hicho cha kwanza na maazimio kadhaa kupitishwa.

Mradi huu kwa hakika ukikamilika utawezesha wale walalahoi wenzetu wa nyasa kuamka wakiwa neema nzito maishani mwao. Ni hivi punde tumekamilisha masuala kadhaa muhimu ambayo yatawezesha mustakabali mzima wa NYAZODE.

Sasa mradi unapiga hodi katika ofisi ya Mbunge wa jimbo la Mbinga magharibi bwana John Komba ili apate taarifa maridhawa kuhusu mradi wenyewe. Na vilevile wazee kama Profesa Mihanjo, hivi punde atapewa maazimio na kuweza kufanya kile ambacho wengi hawakutarajia kufanywa na kundi hili la wazee wa nyasa. Ni hivi punde tu kumemalizika kikao hicho.

ASANTE KWA UHUDHURIAJI WENU NA KARIBUNI S ANA NYASA.

1 comment:

Maoni yako