April 05, 2010

NADHARIA YA PROFESA ZAKARIA MOCHIWA

Wakati mwingine najilazimisha tu kufikiri hata kama silazimiki kufikiria hicho ninachokifikiria.

Natambua umuhimu wa kufikiri kwa wanadamu. Ni busara kujiuliza matatizo mangapi yanapaswa kutatuliwa na mwenyezi Mungu? Ni muhimu kujiuliza hivi sisi ni nani?

Na kwanini basi tupo hivi tulivyo na siyo vile walivyo? Kuna nini, na kwanini wengine wana uwezo wa kubaini kile kinachoweza kubainishwa na wengine pia?

Dunia imejaa mapambano, watu wanafurahia kuishi kwayo na wengine wanalalamika dunia mbaya. Tatizo ni sisi wenye ubaya na maudhi lakini dunia haina ubaya, na tabia mbaya siyo za dunia bali ni mali ya bindamu.
Kumbe ni UTAMBUZI.

*********Ngoja PROFESA ZAKARIA MOCHIWA ATUJUZE ZAIDI*****

NADHARIA YA PROFESA ZAKARIA MOCHIWA


Binadamu yeyote ni matokeo ya ajali tatu.

1).AJALI YA KWANZA NI KUZALIWA

Kila mtu hakupanga kuzaliwa hivyo hakuna aliyepanga kwamba sasa anataka kuzaliwa. Kila mtu alijikuta tu kazaliwa,akalelewa,akakua na kadhalika.

2).AJALI YA PILI NI JINSIA

Profesa Mochiwa alisema ni kwamba hakuna aliyechagua awe na jinsia Fulani,sura Fulani,maumbile Fulani, au rangi Fulani ya ngozi. Ni vitu ambayvo kila mtu anazaliwa anajikuta anavyo.

Katika dunia ya leo tunafahamu wapo wanaobadili jinsia,maumbile,rangi ya ngozi, lakini linathibitisha kwamba hawajivunii hali walizozaliwa nayo.

3).AJALI YA TATU HAKUNA ALIYECHAGUA KUZALIWA MAZINGIRA FULANI

Hii iwe ni nchi nzuri yenye amani,katika nchi au familia yenye utajiri mwingi n.k Kila mtu hujikuta kazaliwa kakulia katika nchi na katika familia Fulani bila utashi wake binafsi. Bila kuchagua kwa vile binadamu huzaliwa katika mazingira ya ajali hizo tatu basi utakuwa ni ujinga kwa mtu kujiona wa maana kwasababu ya faida zilizotokana na ajali hizo huku akiwadharau au kuwacheka wale ambao ajali hizo ziliwaweka katika hasara.

Profesa Mochiwa anasema hivyo sababu ni ujuha kuwatambia wengine kwa kitu ambacho hukukitengeneza wewe, huku ukiwakashifu na kuwadharau wengine kwa kitu ambacho wao pia hawakukitengeza.

Pia ni ujuha kujutia kuzaliwa katika mazingira ambayo ajali zile zimekuweka katika hasara.

Anasema binadamu ni kiumbe anaeongoza duniani kwa uwezo wa kiakili wa kubadilisha hasara za ajali za kuzaliwa kwake zikawa faida pia.

Mfano kutumia uwezo wa kiakili uliozaliwa nao kubadilisha hasara iliyotokana na ajali ya wewe kuzaliwa katika nchi masikini ikawa faida kwako.
********************

NATUMAINI UMEELEWA JAMBO

6 comments:

  1. ukiangalia kwa jicho la ndani, utagundua kuwa kila kitu kimepangwa, katika ulimwengu wa kiroho hama ajali. jifunze juu ya reincarnation mkuu

    ReplyDelete
  2. Nimekuelewa JABALI wangu, nafanya hivyo punde tuuuuuu.

    ReplyDelete
  3. Makala fupi nzuri inayotukakatisha tujihoji.

    Falsafa hii ya Profesa ya Mochiwa ipo katika kitabu gani? Ni Mvumilivu hula mbovu ama?

    ReplyDelete
  4. Mkuu jabali Kamala.
    Nimerudi na maswali, tunahadithiwa sana kuhusu ROHO, nani aliyepanga hizo ROHO? Na kwa mamlaka gani aliamua kuzipanga hivyo?
    Kila kitu kimepangwa na nani? Na kwanini?

    Hii ROHO ipo wapi nami nijionee? Kwasababu kama mtu hakupanga bali alipangiwa KIROHO basi ni AJALI hiyo ndiyo maana Mochiwa anasema wengine wanabadili jinsia, wengine utaona wanachubua ngozi zao. Hii ni AJALI mkuu!! haiwezekani mtu asijikubali vile alivyopangiwa na hiyo ROHO, vinginevyo asingilijichubua au kufanya tofauti na alivyopangiwa.
    ROHO inapangaje haya, na kwanini watu wanakwenda kinyume na walichopangiwa/

    naamini hakubaliani na walivyo, HII NI AJALI.
    wangapi wanatamani kuzaliwa ughaibuni na siyo bongo? AJALI!

    mengo mno maswali hususan hizi habari za ROHO

    ReplyDelete
  5. Markus, umeandika maswali mengi lakini hayo yote hayana maana kwani umesahau kuuliza swali moja "Roho ni NINI?" Ungejua roho ni nini usingeuliza hayo mengine.

    ReplyDelete
  6. Sidhani kama unafahamu theory of Determinism and the concept ya human freedom Kamala manake ulivoandika duuuu.... kwani roho inapingana na mwili? embu tafakari vizuri zaidi juu ya hilo unavoandika sasa hivi imepangwa na Roho au? kweli tafakari kabla hujachukua hatua

    ReplyDelete

Maoni yako