May 12, 2010

BANDARI YA ITUNGI; maji yamepungua


Wiki mbili zilizopita tumehabarishwa wkamba bandari ya Itungi iliyopo wilayani Kyela, imepungua maji kiasi ambacho Meli za MV IRINGA NA SONGEA zimeshindwa kutia nanga hapo.

Kwahiyo habari zilizonifikia hivi punde kumelazimika kutumiwa bandari Kiwira ambayo mara nyigi huokoa jahazi kutokana na kuwa na kina kirefu cha maji.

Hata hivyo kwa mwaka huu hali imekuwa tofauti kwani hata bandari ya Kiwira inakabiliwa na uhaba wa maji. Hali hiyo inatokana na kina cha maji kupungua katika ziwa nyasa.

Bandari ya Itungi Location of Itungi ipo katika Latitudo 9° 34' 60 kusini, na Longitudo: 33° 55' 60 mashariki. Hutumiwa sana kwa usafiri wa ziwa nyasa. Kwa sasa hata bandari ya Kiwira inatakiwa matumizi ya boti zinazokwenda moja kwa moja kilindini kuwapeleka abiria. Yaani meli haiwezi kutia nanga hivyo inasimama umbali kidogo kutoka bandarini hapo.

3 comments:

  1. sasa itakuwa kazi bila safiri, na hizi mvua zimekazana kunyesha Dar tuu. kazi kwelikweli hapa.

    ReplyDelete
  2. Ntarejea hapa baadae.
    Kwa sasa wacha nikuombee.
    Blessings

    ReplyDelete

Maoni yako