May 10, 2010

NDOA ZA MITALA

YANAYOJIRI KWA WANYASA, MALAWI
WIKI hii ndugu zangu wa Malawi wana mjadala mzito, na majadala huo umedumu kwa majuma kadhaa kuhusiana na uamuzi wa serikali kukomesha suala la ndoa za mitala.

Serikali ya Malawi inadhamiri kupiga marufuku suala la ndoa za mitala katika jamii za nchini humo. Sijui zaidi ya hapo kuna nini ila kwa hakika hili ni suala la kuongelea kila mara kuhusiana na mwenendo wa binadamu.
Watetezi wa ndoa za mitala wanadai hiyo ni haki yao na kitendo cha serikali kuingilia kati kutaka kuwapiga marufuku kutooa wanawake zaidi ya mmoja au kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja, ni kuingilia uhuru wao wa kuishi.

Tunakumbuka katika baadhi ya mila na desturi za India wanawake wanaweza kutoa mahali na kuoa, pia kutoa mahali ya kuolewa na zaidi ya wanaume wawili. Hivyo mwanamke ndiye anayepanga hilo, na kulichagua ni namna gani aishi na wanaume wake.

Ndoa za mitala kwa Malawi inaambana na mila na desturi ya makabila yao, kwa kiasi kikubwa kwao ndoa za aina hii ni fahali na kuonyesha ukubwa wa familia n.k, sifa moja kubwa ni kuzaa watoto wengi, na kuwaozesha endapo wapo wanawake au kuwa na watoto wengi na kusifiwa.
Mara nyingi wanawake katika jamii za kabila la Wanyanja na Wachewa hawana kauli sana kuhusiana na maisha ya ndoa hususan wale wanaoishi katika mazingira ya kitamaduni. Au kufanya uchaguzi wa kuolewa na mume gani

Maana wapo wengine nasema hawana utamaduni kwakuwa wanaishi katika mazingira ambayo ni vigumu kuyafafanua kwa utamaduni wao halisi(rejea jamii zilizozuka zamani huko Venice, Italia, na uchambuzi wa Karl Marx.

Hivyo wiki hili katika jiji la Blantyre mjadala siyo haba, na sijui mwelekeo wake utafikia wapi ila serikali imesisitiza kukomesha suala hilo.
Tukienda kwa kabila la Watumbuka, hali nayo siyo tofauti sana sawa na Wahyao.
Hili ni suala ambalo jamii nyingi za Malawi lineendekeza na kuamini kuwa ni uhalali wa maisha yao. Ni wazi wanaamuni kutokana na kurithi tangu enzi za mababu, lakini kama kuna umuhimu wa kuliendeleza ni vema kuangalia nafasi ya maisha halisi kuliko kushadadia tu.
Hata hivyo serikali imefafanua kwamba uwezekano wa kuenea maambukiz ya ukimwi kunatokana na ndoa hizi, inaelezwa wkamba wengi wanaolewa/kuoa kisha kuachwa/kuachana na kujikuta wakiwa wameathiriwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi.
Na zaidi inaelezwa kuwa kunakuwa na ongezeko la wajane au watu walioathiriwa kisaikolojia kutokana na ndoa hizo. Wengine ni mabinti wadogo ambao huozeshwa kulingana na mila na desturi.
Ni matumaini yangu Usia Nkhoma utachangia hapa, Vincent Kumwenda, Alley Kapito.... Lol! nchito ilipo bambo..... just for u Sophie Moyo.

TUJIULIZE
Ndoa za mitala ni hatari sana?
Kuna athari za ndoa za mitala?
serikali inaingilia uhuru wa kuishi?
Binadamu tunao uhuru kiasi gani?

4 comments:

  1. Serikali iangalie na kufikiria kwa undani inachotaka kukikomesha kama kitakomesheka kwa kukomesha ndoa za mitala.

    Kwa mbaaali naanza kuona serikali hii inapoelekea. Chonde wasifikie walikofika ndugu zetu huko Arabuni.

    ReplyDelete
  2. Anonymous11 May, 2010

    Markus, pengine napo pitia hii blogu yako nafurahi sana kwa kuwa nami ni mwiongoni wa watanzania wenye asili ya Nyasa (si Malawi). Hata hivyo, mara zote ni kama mada nyingi na hata blogu ambazo zinaunga na hii ya kwako inaonekna ni za Malawi.

    Pengine labda kama inawezekana kupata habari na mijadalo inayohusu maeneo yetu kuanzi huko Ukisi, LUNDU, NJAMBE, PUHULU, LIULI, NKALI, HONGI, LIPINGO, LUNDO, NGINDO, CHINULA, NDENGELE, MBAMBABAY, KILOSA, LINDA, LIKWILU,TEMBWE, MBANGA MAWE, CHIULU, UNDU, MTIPWILI, CHIMATE, KWAMBE NGO'MBO mpaka CHIWWINDI (mpakani mwa Tanzania na Msumbiji) ingekuwa ni faraja zaidi kwa wale watokao huko.

    Binafsi nafahamu pia kwa maeneo hayo bado kuna desturi zinazofafana na ndoa za mitala ambapo wanaume utakuwa anaweza kuaga mkewe asubuhi sana kuwa anakwenda shambani au ziwani, lakini anaenda shamba la "nyumba ndogo" (wanaita madaba)huko atalima, na akitoka hapo anaweza kwenda ziwani na kupata samaki kadhaa (ntungo) lakini akaishia nao huko huko "madaba" ambapo atakupikiwa ugali wa muhogo na wale samaki wake wote, atakua na kupumzika kwa masaa kadhaa kabla ya kurejea kwa mkewe.

    Akifika kwa mkewe anakuwa yu mikono mitupu lakini anasema alipitia ziwani na hakuweza kupata kitu chochote hali ya ziwa bado ni mbaya.

    Maisha ya jinsi hiyo yalianza kwa wazee lakini sasa imekuwa kama ni wimbo wa taifa hasa kwa vijana, na ule utamaduni wetu wa kule wa "Mganda" na Chioda unachangia sana kuongeza kasi ya maambukizi kwani katika kipindi hicho wanaume au wanawake huwa wanasafiri kwenda kucheza ngoma kijiji kingine na wanakaa huko pengine zaidi ya siku tatu...na huko inakuwa kula kunywa na kulala na starehe nyinginezo.

    ReplyDelete
  3. Ujumbe umefika mwanawani. Yote yamo kichwani. Sukrani kwa kumbukumbu MANGO,NKILI,HINGA,LIWETA,MBAHA,NDUMBI,LITUHI,MANGO, kwinginekoooo

    ReplyDelete
  4. Anonymous26 May, 2010

    zikomo kwa mbili Anonymous hapo juu

    ReplyDelete

Maoni yako