May 06, 2010

KAZI UKIIPENDA,ITAKUPENDA

                                             Kazi ni kuipenda
Maisha ndivyo yalivyo lakini mpangaji ni wewe. Ukiipenda kazi yako nayo itakupenda. Ukiithamini kazi yako nayo itakuthamini, ukiheshimu kazi yako nayo itakuheshimu.
Kazi ni kazi bora mkono kwenda kinywani, lakini siyo kazi yenye dhuluma ukadai bora mkono unakwenda kinywani, bali kazi ni ile halali na uifanye kwa uhalali.


Kazi yoyote ni kuipangilia, na zingine hazina ofisi ambayo utakaa kuandika kwa kalamu ya wino. Kwetu hapa nyasa kazi yetu na ofisi yetu ni mtumbwi ambao kalamu yake ni ngalawa/kafia.
Kazi hii ni ngumu lakini ndiyo inayoweza kutupatia kipato na kupanga maisha.
Kazi ukiipenda nayo itakupenda, hata kama ni ndogo aghalabu inakupa heshima.
Ndipo unapomkumbuka Vilfredo Pareto, mchumi wa kitaliano katika '2080 Theory', kwamb asilimia 20 ya mipango yako ni sawa na asilimia 80 ya matokeo'.


Ukiifanya kazi kwa bidii,maarifa na kwa asilimia zote, itakuletea ufanisi. Ufanisi unatokana na juhudi ndiyo maana hatuachi KUVUA SAMAKI. Najua jamaa zangu wa pale bandarini Chilumba, Malawi hawaachi na serikali yao imewaletea zana mpya. Hongereni. Lakini sisi tunatumia mitumbwi ya zamani na tuna uhakika wa kufanikiwa labda.

2 comments:

  1. Ukiamini kufanikiwa basi utafanikuwa!Na kweli ukipenda kitu chochote kile nacho kitakupenda.

    ReplyDelete
  2. Nimekupata Mzee Mcharuko. Kila kitu ni wewe mwenyewe tu.

    Sengwili sana.

    ReplyDelete

Maoni yako