May 03, 2010

KWAKO KAKA MUBELWA BANDIO

 Ndugu Wanablogu, nimeamua kwa dhati kuchukua maoni haya ili tujifunze jambo. Soma maoni hayo ambayo nimeyatoa kwa Mchungaji Koero kuhusiana na mada ya ANAPOZUNGMZA MWENDAWAZIMU...... sasa mimi maoni haya hapo chini, halafu utasoma maoni yangu mwishoni yatokanayo...


Mzee wa Changamoto said...

At least SHE IS TRYING (according to you Anon)

Ungejua THAMANI HALISI ya kuandaa alichoandaa, ungetafakari ulichoandika

April 30, 2010 4:22 AM

Anonymous said...

Mzee wa Changamoto. I didn't mean anything offensive but if you read her article, it is obvious that she is trying too hard. Sasa wewe unakurupuka kum-defend. Why? Do you know her? Is she your ex???

This is the problem with you TZ bloggers. You don't tolerate any opposing views. If what you are writing is intended to be DOGMA and never be questioned, then there is no point of even having these stupid blogs of yours. You make me very sad when you do this. That is why I will just stick with Jamii Forums and Wanabidii where free speech is acknowledged na siyo nyie marastafari FEKI...Everyday Luciano said this, Lucky Dube said this...Bullshit. These were drug addicts and why do you keep on quoting dem zombies? Did they even know what they were talking about???

This is the last time that I will vizit a Tanzanian blog - with an exception of Professor Joseph Mbele, Kamala Luta, Matondo Mzuzulimwa and Kaluse who doesn't mind to be questiond. May be you should change your blog to "The way I see your opposing views is the problem"

April 30, 2010 8:53 AM

Mzee wa Changamoto said...

Well!! Anon

I guess you're on the same page as us. Kwamba UNAPINGA SISI KUTOTAKA KUELEZWA UKWELI WAKATI WEWE MWNYEWE HUTAKI KUELEZWA UKWELI. That's wonderful.

Kumbe nawe unapinga unalotenda? Kama hudhani kuwa kukosolewa ni kosa nawe ungenikosoa niliyosema nami nikakukosoa kwa uliyosema na hakuna shaka kuwa kuna wakati mwenye kusimama katika FIKRA ZA KWELI ATAKUWA MUELIMISHAJI KWA WENZAKE (si lazima anayekosoana naye). Sio kufanya ulivyofanya kwa kususa kwenda mahali ambapo hujakaribishwa na kutokuwepo kwako hakutapunguza lolote kwani wewe unakuwa mmoja wa MNAOKIMBIA UKWELI.

Nakwambia wewe si wa kwanza na hautakuwa wa mwisho

Sasa wewe unayepinga suala la kukosolewa unasema hutatembelea blog ambazo UKIKOSOA NAWE WAKOSOLEWA.

Kama ningekuwa naogopa kukosolewa ningekuwa nina-moderate maoni kwenye blog yangu na sifanyi hivyo kwa kuwa ukiandika FIKRA ZAKO nami NTAANDIKA ZANGU.

Najua unajidanganya kusema hutatembelea blog hizi kwani natambua fika kuwa utarejea hapa kusoma nililokujibu.

Kuhusu Lucky Dube, Luciano, Bob, Bushman, Burning Spear na yeyote yule nimsikilizaye na kuandika juu yake sitaacha. Nitafanya hivyo kwa kuwa wewe unayewaona kuwa si watu wema ndiye uonaye na si mimi. Na siamini kuwa mimi ni mtu mwema pia, bali najua wewe, wao na mimi sote tuna wema.

Kauli yako kuwa "you are trying too hard" inajieleza vipi? Inakosoa, inavunja moyo, inarekebisha, inaonya ama?

Labda ungeandika kwa ufafanuzi zaidi ingesaidia. Na ndio maana nikasema kuwa "at least she is trying" kwa kuwa nami najua inachukua muda gani kuandika post kama hii na kubwa ambalo ningefanya (na ambalo nimeshafanya mara nyingi) ni kueleza kile ninachoamini hakiko sahihi katika alichoandika na sio kutothamini kila kitu (ikiwa ni pamoja na muda wake)

Tutakutana hukohuko kwa Profesa Mbele, Profesa Matondo, Kaka Kamala, Kaka Kaluse na wengine ambao utawatembelea (nami nawatembelea pia) na nakuhakikishia kuwa huko utapata uelimishaji tosha (kama nipatavyo mimi) na kwa kuwa hata sehemu ya post zangu huwanukuu hao.

Siko pale KUTAFUTA WATEMBELEAJI (hasa wasiojitambulisha) na nitaendelea kutimiza ninalotimiza. Nakurejesha kulekuleeee ulikokataa kwa Bob kuwa "Dready got a job to do

And he's got to fulfill that mission

To see his hurt is their greatest ambition, yeah!

But-a we will survive in this world of competition,

'Cause no matter what they do

Natty keep on comin'through,

And no matter what they say,

Natty de deh every day."

Jina la blog litabaki kuwa hivyo lilivyo na wewe kuliona visivyo NDIO TATIZO.

Hahahahahaaaaaaaaaaaaa

Good luck

*******************************************************
MAONI YA MCHARUKO a.k.a Mzee wa Nyasa

Kitu kimoja nisichokubaliana nacho ingawa sina hiari nacho ni kuwanyima fursa WASIOJITAMBULISHA yaani ANON. Mimi lazima niseme wazi kwani kawaida kuna mambo kwangu siyo faragha. Nilikuwa nje ya blogu kidogo lakini sikujua hali hii hadi nilipoambiwa nisome VUKANI katika mada hii.
Hakijanishtua kitu ila namna ambavyo sisi watanzania tunavyojaribu kutokubali mtoa hoja na kuangalia yeye binafsi.

Kwa mfano ANON anataja kuhusu WANABIDII, kwangu mimi siwezi kupoteza muda kuchangia sana mtandao huu ingawaje waandaaji wake ni RAFIKI zangu, tunafahamiana na nilisema waziwazi pale SOMA CAFE mikocheni. Kusema WANABIDII ndipo penye mjadala huru ni ujinga mwingine ingwaje naheshimu sana maoni ya wote. Kuna mambo yanajadiliwa kwa porojo,hofu,wehu,udaku, na vitu vingine. Najua yapo mambo mazuri ambayo yanajadiliwa ila niliamua kukaa kando na mgomo wangu wa kutojihusisha uliisha hivi karibuni kuhusu timu yetu ya taifa.

Hivi mada inayomzungumzia HEKAYA ya wazee wetu na kuwa EX yanahusiana vipi? Hii ni wazi tunashindwa kuheshimu kazi za wengine, na huu ndiyo utamaduni unaotumiwa sana na watanzania. Sasa JamiiForums anayosema ina nini? Mbona nasoma mimi sioni kitu jamani au? Mnisamehe kwa mcharazo huu, sitaki kufuata mkumbo bali nataka kitu kilichokamilika, kwahiyo huyo ANON asitake kutufundisha namna ya kuingia katika mijadala.

Kwa majibu ya Mzee wa Changamoto kwamba hatuandiki ili tusikosolewe, bali tunaandika ili kuelemisha, kwahiyo inatakiwa kupewa thamani ya kile kinachoandikwa. Lakini siku hizi kuheshimu anachofanya mwenzako hususan maoni hayo yananichafua ingawa nayaheshimu.

Tunaongelea MANTIKI, FANI na MAUDHUI. Lakini majibu ya ANON yanaonyesha wazi wazi kuwa wapo watu wenye AKILI ZENYE MATEGE. Sijui niseme nini kwa ustaarabu lakini hawa pia ni watu wanaofahamu wanaotufahamu. Kwa kawaida mimi hutumia muda sana kuwasoma kisha kuangalia aina ya uandishi. Sihabatishi ila nasema ni watu wanaofahamika kila siku kwetu, naweza kusema kwa kiasi fulani nimebahatisha huyu ANON ni .....................(sitataja, naweka kwapani)

TANZANIANS BLOGGER? hivi kusema hilo ni tatizo la wanablogu wa Bongo kuna mantiki gani na mada husika. Kwanza huko Jamii Forums kuna lipi la ajabu? Au Wanabidii kuna lipi lenye bidii mnayoizungumizia? Mbona mimi sioni kitu? Sasa ANON pamoja na kuheshimiwa lakini lazima uanze kujiheshimu JITU LENYE UHAKIKA HALIMCHUNGULII MKEWE. Kwanini ufiche utambulisho wako kama kweli UNAAMINI NA KUJIAMINI kwa maoni yako kuwa ni WEWE?

KWAKO MZEE WA CHANGAMOTO; kwa maoni yako uliyoandika nipo nyuma yako nakuunga mkono, tena kwa asilimia hadi za mizoga ya ndugu zangu wa huko Lilongwe na mizoga iliyopo Bongo iliyoza miaka hiyoooo. Hakuna aliyelazimishwa kusoma, vinginevyo itakuwa ni hulka ya mtu mwenye AKILI ZENYE MATEGE.

Mzee wa changamoto; kumbuka Ben Mtobwa katika kitabu chake cha NYUMA YA MAPAZIA anasema 'waigizaji ni wengi siku hizi, maisha yao yamejaa maigizo, wnajifanya hawajui, lakini najua wanaigiza'.

Mcharuko kwa ANON;
nasema hivi, ANON huyo ni sawa na wale wanaona kinyesi kimezungukwa na inzi halafu wanatema mate kwa kinyaa huku wakisahau kuwa WANATEMBEA NA VYOO kila waendako. Ukibisha nitakuuliza ANON hujabanwa na mavi wewe? hujajamba wewe? Hilo siyo choo a.k.a MAVI?
Kabla hujatoa maoni ya ujumla angalia somo husika ili uhitimishe kwa ujumla.
Namaliza kwa ujumbe huu kwa huyo ANON; WHEN MY HEART CAN'T BEAT NO MORE, I HOPE I DIE FOR PRINCIPLE AND BELIEVE THAT I LIVED FOR.

Ni ujumbe mahiri.

ASANTE MZEE WA CHANGAMOTO kumwelimisha ASIYEJIAMINI na kujificha vichakani.
UBARIKIWE. Usisahau kumsikiliza Dr Dre katika 'Forget About Dre'' kaka Tupac katika 'HOW DO YOU WANT IT' au kaka Clifford Harris a.k.a T.I katika 'WHATEVER U LIKE'

3 comments:

 1. Nilikosa ushiriki mzuri wa jambo kuuuuubwa na la muhimu kama hili. Nipo katika maandalizi ya post ya changamoto za kublog. Hii ni reference nzuri sana.
  Kabla sijaondoka niseme tu, blog ni uhuru wa mwenye blog kuamua kipi akiweke.
  Mchungaji Koero, Lundu Nyasa, Kaka Mutiba na wengine wooote tutaendeleza libeneke pasipo kujali nani anatuheshimu, nani anatudharau, nani anatudhihaki, maana hatufanyi haya ili kupata umaarufu bali kutoa yaliyopo vichwani mwetu.
  Alamsiki.

  ReplyDelete
 2. message sent.

  Penye wakubwa hapaharibiki neno

  ReplyDelete
 3. Amani, Heshima na Upendo kwako "Mzee wa Mcharuko".
  Kwanza natumai umeona kuwa mawasiliano yangu katika blog yamekuwa ya kusuasua kwa siku za karibuni. Ni majukumu tu.
  Na nirejee hapa.
  KWANZA NI SHUKRANI ZA DHATI kwa kuweza kuweka bayana msimamo wako kuhusu hawa ma-anon ambao wamekuwa sehemu muhimu saana ya blog lakini bado wapo wanaotumia umuhimu huo kuchafua hali ya hewa. HAWA WAPO HATA BUNGENI.
  Lakini pia niungane nawe kuwa kwa "style" ya uandishi, naweza hisi kuwa mtu aliyeandika vile ni mchangiaji wa muda mrefu ila kwa kuwa aliamua KUMVUNJA MOYO Da Mdogo Koero, akaamua kutojitambulisha.
  Kwangu nawaza lengo hasa la kumvunja moyo mtu ni lipi? Na kwanini mtu (ambaye pengine hatambui ugumu wa kuoanisha fikra za kile uwazacho na posts za watu mbalimbali) anaweza kukosa hata thamani ya muda wa aliyejitolea kuandika lililo jema.
  Yule ni msomaji mzuuuri saana na naweza kusema hivyo baada ya kuandika kwa hasira juu ya Luciano na Lucky Dube lakini naweza pia kuelewa ni kwanini alionekana kuwachukia hawa (kati ya wote niandikao). Najua nilishaandika kuhusu Luciano kuhusu wimbo SITTING AND WATCHING (utunzi wa Dennis Brown) ambaye alisema "sitting and watching fools by themselves when they should always thinking of getting to know themselves" na asichojua ni kuwa hata kina Prof Matondo, Prof Mbele, Kaka Kamala na Kaluse walishasema kuwa hawatabishana na wasio majina. WANAWAANGALIA WANAVYOJIPUMBAZA KWA MAONI YAO BADALA YA KUJIFUNZA KUJITAMBUA. Pia niliandika kuhusu Lucky Dube aliposema "if you can't say something good about somebody, just SHUT UP" na tunawea kuona kuwa huyu hakuwa na lolote zuri kwa Da Koero. Na alistahili kunyamaza.
  Leo hii anasema hatatembelea kwa Koero kwa kuwa nimemsema na ataenda kwa Kina Prof Mbele, Prof Matondo, Kaka Kamala na Kaka Kaluse na analosahau ni kuwa hawa wote HAWAJANIFUNGIA KWENDA HUKO NA NIKIKUTA ANAPOTOSHA NTAMSAIDIA KUMUWEKA SAWA.
  Kwa mantiki hiyo, ajiandae kukimbia kila mahala ambako atakuwa akipotosha kwani kila nitakapomkuta ntarekebisha.
  Na analosahau ni kuwa SISI HATUANDIKI MAKALA KWA AJILI YA WATU WOTE, TWAANDIKA KWA AJILI YA WAHITAJI na yaonekana yeye si mhitaji (kama ambavyo hatumhitaji sisi) na hivyo kususa kututembelea ni kutuondolea makapi na kutufanya kubaki na "pure product" ambayo tunaweza kui-handle na kuisaidia.
  Ila najua atarejea tuuu iwe kwa jina jingine ama vingine, lakini kwangu jina si kitu, bali maudhui. Haijalishi atakuja kwa jina gani, akiwa na maudhui sawia tutasonga, na yasiyo sawa, tuta-changamoto-ana
  Blessings

  ReplyDelete

Maoni yako