May 30, 2010

UMEWAHI KUFIKIRIA HILI KUHUSU SISI WANADAMU????/

KUNA MTU UMEWAHI KUMCHUKIA?? UNADHANI KUNA WATU WAMECHAGULIWA NA MUNGU??
......Ndiyo wapo wanaofikiria hilo,,,
Ndiyo maana wanaona wako karibu na Mungu.......... NINACHOJUA na kukiamini ni kuwa kila kiumbe duniani ni CHAGUO LA MUNGU, maana bila Mungu hakuna kitu kinachoweza kuwepo. Ndiyo maana hata SHETANI ni chaguo la Mungu, kama siyo chaguo la Mungu basi asingeumbwa.

SASA......... Mungu alitupatia akili na utashi ili tujue mema na mabaya kati yetu ili tumpendeze yeye tu. Twaweza kuishi hata bila chakula katika mazingira fulani lakini bila Mungu hatuwezi kuishi. Najua kila mtu duniani hata wewe unayesoma hapa ni CHAGUO LA MUNGU.
Waungwana nimeipenda hii kitu ya kutoka kwa FALSAFA YA ISANGO inayoandikwa na Josephat Isango au Misango.
Stori ya kipengele cha kukosoa dini leo nimeweka kando aiseeeee., lakini hata hii imekuwa poa. Mtani Fadhy upo hapo???? Da Mija, unasemaje, mtakatifu mungu wa wapare.... Ruksa kubishia Lol.....

4 comments:

 1. Mtani sikumbuki mara ya mwisho nilimchukia mtu lini. Nadhani wakati nasoma pengine sekondari. Ninachokifahamu maishani ukiendekeza tabia ya kuchukia watu unakuwa mtumwa. Mi wala siutaki huo utumwa.

  Nakubaliana nawe kila mtu ni chaguo la Mungu hakuna exceptionals hapa.

  ReplyDelete
 2. Kwa hiyo bila Mungu tusingekuwa na wanablog...aisee, kumbeeee,

  Nakubaliana na wewe 100% Lakini, nakumbuka nilishawahi kumuuliza mama, (baba alishafariki zamani nadhani nikiwa na miaka 10 tu.)
  Nilimuuliza hivi, Kwa nini Mungu aliumba shetani, na kwanini alimtupa hapa duniani ili atupotoshe halafu twende motoni?

  Na je tukisema Mungu alikosea tutakuwa tumekosea.......
  Nakumbuka nikichalazwa bakola za kufa mtu, eti nimehoji mamlaka ya mungu ambapo hairihusiwi kuhoji lolole kuhusu yeye.

  Hebu nijinyamazie nisije nikaambiwa kuwa nimekufulu bule.

  ReplyDelete
 3. Mimi sijui na siona haja ya kumchukia mtu kwani napoteza muda wangu bure. Na tukumbuke ya kwamba kila kitu ndiye aliviumba na sisi sote ni watoto wake. Kwa nini kuchukiana. UPENDO DAIMA!!

  ReplyDelete
 4. Mtani umesema kweli, yaani ni bonge la mzigo ambalo kwahakika unaweza hata kujishangaa unabeba zigo kuliko guta au lile la kuli.

  Maisara, nikwambie kitu, wengine ilitung'arimu sana suala hili la kuhoji mamlaka ya mungu enzi tukiwa utawa, sasa ikasemwa huyu mwanzoni tu yuko hivi itakuwaje tuendako. Naungana na wewe kuna maswali lukuki ya kujiuliza kuhusu Mungu, na zaidi yapo mengine ambayo tunaambiwa yanatokana na mungu kumbe wapo watu wametengeneza mambo kwa kivuli cha mungu. Ngoja tutaonyesha machache tuendako. Tena ulipocharazwa bakora ulionewa bureeee na wakati huo ndiyo tunaumbiwa jina la mungu kana kwamba ni jitu la kutisha.

  @Yasinta, UPENDO DAIMA

  ReplyDelete

Maoni yako