Sehemu ya jengo la madarasa katika shule ya Sekondari Lituhi, mjini Lituhi. Kwa sasa hali ya mabadiliko imekuwa kubwa kutokana na shule hiyo kukabidhiwa kwa serikali ambapo mwanzoni ilikuwa ikimilikiwa na wazazi ambao waliamua kujenga sekondari hiyo kwa lengo la kuondokana na kero ya ukosefu wa elimu kwa watoto wao.
Hosteli za shule ya Sekondari ya Mbamba bay, mjini Mbamba Bay. Hatua hii itasaida kuondoa ukosefu wa mabweni katika shule nyingi za Kata katika wilaya ya Nyasa. Kwakuwa sekondari ya Mbamba Bay ni ya Kata basi inaweza kuchukuliwa kama mfano wa shule zingine ili kuondokana na kero mbalimbali za elimu na kuwafanya wanafunzi wasome kwa utlivu wakiwa na maeneo mazuri ya kusomea.
Jengo la madarasa matatu katika shule ya sekondari ya Linda iliyopo nje kidogo ya mji mkuu wa wilaya ya Nyasa, Mbamba Bay. Ujenzi wa madarasa hayo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2013. Ambapo Ujenzi wake ulianza katika mwaka fedha 2008/2009. Hii ni hatua nzuri ambayo inahitaji msukumu zaidi ili kukamilisha huduma za elimu kwa wakazi wa mji wa Linda na wilaya Nyasa kwa ujumla.
Madrasa ya shule ya sekondari ya Wukiro, iliyokarabatiwa kwa baadhi ya vifaa vya LCDGC, ambapo ukarabati katika majengo hayo haujakamilika. matarajio yake ni kukamilishwa mwanzoni mwa mwaka ujao 2013.
PICHA ZOTE NA HOOPS KAMANGA, Nyasa.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako