December 22, 2012

PhD YA KWANZA KUANDIKWA KWA LUGHA YA KISWAHILI UDSM

Na Honorius Ngachipanda, Mbeya

Katika hali ambayo inaleta matumaini makubwa kwa wapenzi wa lugha ya Kiswahili, taarifa wkamba Dk. Metho Samweli amefanikiwa kuandika Thesis yake ya PhD ya somo la Kiswahili kwa lugha ya Kiswahili ni za kusisimua.
Kwa mujibu wa gazeti la THE HILL OBSERVER la Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Method Samweli amekuwa mhitimu wa kwanza wa Chuo hicho kuandika Thesis ya PhD kwa lugha ya Kiswahili. The Hill Observer limeeeleza kuwa kwa muda mrefu sana wahitimu wote walikuwa wakiandika thesis zao lwa lugha ya kiingereza. 
Lakini Dk Method Samweli mwenye miaka 32 ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu (UDSM-DUCE) ametunukiwa PhD hivi karibuni wakati wa sherehe za 42 zilizofanyika kwenye ukumbi wa MCCC (Mlimani City Conference Center).
Mkuu wa Idaya ta fasihi, Mawasiliano na Uchapishaji katika Idara ya Kiswahili ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, Dk. Shani Omari alisema kuwa kabla ya thesis ya Dk method Samweli, hapakuwahi kutokea Thesis yoyote iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili Chuoni hapo. 
Aidha, Chuo Kikuu cha Dar es salaam kinafuata nyayo za Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambacho tayari wapo wanafunzi kadhaa walioandika thesis zao lugha ya Kiswahili. Miongoni mwa wahitimu wa PhD waliofanikiwa kuandika Thesis zao kwa lugha ya kiswahili, ni Mohamed Seif Khatibu ambaye ni waziri mwandamizi na kiongozi wa siku nyingi ndani ya CCM.

WASIFU WA DK. METHOD SAMWELI
Alijiunga sekondari ya Ndanda, kisha akajiunga na UDSM mwaka 2002 hadi mwaka 2006 alipomaliza masomo yake ya B.A with Education na kuwa mhadhiri msaidizi wa UDSM-DUCE. Kati ya mwaka 2006 na 2008 alimaliza masters katika masomo ya Linguistic hapo hapo UDSM. 

2 comments:

  1. Ni jambo lenye kusisimua mno na kutia moyo kwa wapenzi wote wa lugha ya Kiswahili.

    ReplyDelete
  2. mtani hili nimelipenda sana na hakika linahitajika sana katika nchi yetu. Nakuunga mkono

    ReplyDelete

Maoni yako