Na John Chitanya, Nyasa
Naandika baada ya kufanya ziara fupi kutembelea shule ya
sekondari ya Monica Mbega iliyopo Kata ya Mbaha katika Tarafa ya Ruhuhu.
Nilianza safari yangu katka kijiji cha Lundu kuelekea Mbaha, ambapo umbali wake
ni kilimita 1, niliwasili shuleni hapo yapata saa asubuhi.
Lengo la safari hiyo ni sehemu ya mkakati wa kutembelea
shule zote za Kata katika Tarafa ya Ruhuhu, kisha shule za Tarafa ya Ruhekei
kwenye wilaya mpya ya Nyasa. Nilipowasili shule hapo nilikusudia kuangalia mazingira ya
shule na namna gani walimu wa shule hiyo wanavyowasilia katika uwajibikaji wao
kwa wanafunzi na namna gani wanafunzi wanawajibika kwa walimu wao ili kujenga
nidhamu na mafanikio ya shule.
Nidhamu baina ya mwalimu na mwanafunzi ndio msingi mkuu wa
kulefa mafanikio ya shule yoyote.
Mpaka naondoka shuleni hapo saa moja na nusu sikufanikiwa
kumuona mwalimu yeyote hata wa zamu hakuwepo, mazingira ya wanafunzi nao wapo
kama wapo msibani hakuna shughuli za usafi wa mazingira. Nilijaribu kumhoji mmoja wa wanafunzi kama wamefanya ‘roll
call’, nikaambiwa muda bado haujafika. Wakati huo ilikuwa saa moja na robo. Mpaka
muda huo nilikuwa na wanafunzi wasiozidi 50.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mango, wilayani Nyasa. Picha kwa Hisani ya Tanzglo |
Na kati yao hapakuwa na mwenye saa. Picha hiyo unatarajia
patakuwa na hali nzuri kimasomo, wajibu na nidhamu kati ya mwalimu na
mwanafunzi? Kwahiyo hali nzuri ya kitaaluma kwa shule kama hiyo sio
jambo linaloweza kutokea, kwa vile mwanafunzi hurithi tabia za wakubwa naamini
wanafunzi watakuwa katika hali gani kitabia na kitaaluma toka kwa walimu hao? Kama mwalimu ni mvivu kuwahi shule unatarajia atapanda mbegu
gani kwa wanafunzi wake? Nilipojaribu kutaka kujua kama walimu wanakaa mbali na
maeneo ya shule niliambiwa wote wanakaa ndani ya mita 100 toka shuleni hapo. Je unatarajia nini kwa shule
kama hiyo?
Nilifanya ziara hiyo kwakuwa mwezi wa pili nilikuwa katika
kikao cha tathmini ya matokeo ya mitihani ya taifa kwa kidato cha pili na nne.
Nilienda kwa niaba ya mzee kwa wanafunzi. Katika matokeo ya kidato cha pili
walikuwa wanafunzi sio chini ya 47, lakini waliovuka wastani ni wanafunzi
watatu tu. Katika matokeo ya kidato cha nne hawakuzidi wanafunzi 37,
lakini waliopata vyeti kwa daraja la nne kwa pointi 29-33 ni wanafunzi 6 pekee na wanafunzi waliobaki walifeli.
Wakati ule mkuu wa shule alijitetea kwenye kikao cha
tathmini kuwa shule haikuwa na walimu
wa kutosha kwani walikuwa watatu tu. Kwa sasa shule hiyo ina walimu 8
bado hawatoshi. Kama walimu 8 hawafiki darasani kwa muda mwafaka wakiwa
walimu 20 itakuwaje hali ya shule hiyo? Sitakosea nikisema walimu hao ipo siku
watafika shuleni saa sita mchana kwa kufuata muda wa vipindi vyao tu? Leo nimekumbuka msemo wa walimu wa siku hizi ni
walimu wa bongofleva wanafika shuleni wamevaa suluali za jeans. Na wao
wanajitetea kuwa ualimu sasa sio wito bali kazi, na kama wito ulikuwa zamani
sana. Sijui, natafakari tu.
• John
Chitanya, ni mwandishi na mwalimu wa Miracle Center iliyopo Songea. Maoni: 0718
005557
ReplyDeleteHere is my web-site how to win the lottery