September 02, 2013
UTATA WA FURSA ZA AJIRA NYASA - MKUU WA WILAYA YA NYASA APIGWA VIJEMBE MITAANI
Mwandishi Wetu,Mbamba Bay
Nyasa ni wilaya mpya ambayo imejaa changamoto nyingi. Mwandishi wetu anatuarifu hali halisi juu ya ajira katika wilaya mpya ya Nyasa.
Wakati wa Sensa katika Kata ya Mbamba Bay mjini walijaa wageni ambao ni watoto au ndugu wa wakubwa toka maeneo ya Dar es salaam,Mbeya, Mwanza.
Jambo jingine ni kwamba kuna malalamiko askari wamechaguliwa watoto wa wakubwa ambao ni wageni.
Pia wafanyakazi wa Halmashauri 96% ni wageni.
Hivyo Mkuu wa wilaya aliamua kuitisha kikao cha wazee kuomba ushauri juu ya Vijana wanaomtukana lakini akaambiwa mbona hata askari wako nao wanakaa vijiweni huenda ndio wanaokutukana!
Hata hivyo mkuu wa wilaya ameahidi kufanya marekeboshi kwenye malalamiko hayo. Kwa kwasasa wameamua kutoa ajira ya kufyatua tofari 100,000 kwa kila Kitongoji ya kujengea majengo ya Wilaya.
Madhumuni
kumbukumbu,
maisha,
Nyasa,
Uchumi
WASIFU: Mwandishi wa Habari,Tawasifu,Mhariri na Mchambuzi wa Vitabu,Siasa, Utamaduni, Michezo,Afrika, Kimataifa,Mshauri wa Habari na Mikakati. TUWASILIANE: mawazoni15@gmail.com, lundunyasa@yahoo.com. WHATSAPP; +255 719226293/SMS; +255 764 936655
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako