December 22, 2013

SERIKALI KUJENGA KAMBI ZA JESHI WILAYA YA NYASANa Mwandishi wetu, Mbamba Bay 
SERIKALI imepanga kujenga kambi mbili za jeshi ili kuimarisha suala la ulinzi na usalama katika wilaya ya Nyasa, ambayo imeundwa rasmi mapema mwaka huu.  
Kwa mujibu wa tarifa zilizoifikia mtandao huu ni kwamba serikali imekusudia kujenga kambi ya kijeshi katika kijiji cha Ng’ombo kilichopo kilomita chache kutoka mji Mbamba Bay. Kijiji cha Ng’ombo kipo kilomita chache pi kutoka mpka wa Tanzania na Msumbiji, kikitengenishwa na vijiji vya Chiwindi, Mtupale na Chimate.


Aidha, serikali pia imekusudia kujenga gereza la Wilaya ya Nyasa katika kijiji cha Lundo, ambacho kinafahamika zaidi kwa kuwa moja ya eneo muhimu lililowahi kutumika kuwahifadhi wakimbizi wa Msumbiji. 

Kijiji cha Lundo kipo katika mandhari mazuri na kitakuwa na msaada mkubwa wakati wa shughuli za kuendeleza jamii ikiwemo kuhifadhi wafungwa watakaokutwa na hukumu katika maeneo mbalimbali.

Kufuatia hilo, pia shughuli za maendeleo ya jamii na uchumi zinatarajiwa kuongezeka katika kijiji hicho pamoja ja kuwasili wafanyakazi na ongezeko la hudumu muhimu za jamii.

TINGI
Katika hatua nyingine  serikali inaendelea na mradi wa kujenga kituo kidogo cha Polisi na Mahakama katika kijiji cha Tingi ambao unatarajiwa kukamilika mapema mwaka 2014.No comments:

Post a Comment

Maoni yako