December 22, 2013

UHABA WA SAMAKIMwandishi wetu Vitus Matembo amezoea kula samaki huko Nyasa, lakini kwa sasa analalamika kuwa kuna uhaba wa Samaki. Katika hali ya kawaida miezi ya Septemba, Oktoba mpaka Novemba kunakuwa na uhaba wa samaki wa aina fulani. Kwa wanyasa kuna samaki wanawapenda sana, lakini wanapotoweka basi inakuwa tatizo. 

Hivyo kwa sasa samaki wanaopatikana zaidi ni maarufu kama MCHUKWA, lakini samaki aina ya Kambale upatikanaji wake ni mgumu kipindi hiki labda kuanzia januari. Na kwakuwa wanyasa wamezoea kula samaki wanono basi tusmishangae ndugu yetu Matmebo akilalamikia kukosekana kwa samaki anaowapenda.
Ndiyo Nyasa yetu, raha na changamoto.
Kwa sasa ununuzi wa Kambale unaweza kuuziwa kipande badala ya kambale mzima. Hapo ni kipande cha Kambale akiwa tayari kwa kuuzwa. KARIBUNI NYASA


No comments:

Post a Comment

Maoni yako