Mwandishi Wetu, Mamba Bay
BAADA
ya kutegemea shughuli zake kufanyika wilayani Mbinga, hatimaye sasa wilaya ya
Nyasa imeanza kushughulikia majukumu yake.
Miongoni
mwa majukumu hayo ni utumishi, ardhi, na mengine yanayohusu maendeleo. Hapa ni
sehemu ya majukumu yaliyoanza kufanyiwa kazi;-
Tambua
kuwa Wilaya yako mpya inatoa huduma karibu 99%. Idara zote zipo sasa Nyasa.
Vyeti
vya kuzaliwa vinapatikana kwa bei nafuu. Wakubwa - Tsh.10000, na watoto wadogo
Tsh.5000.
Leseni
za biashara zipo. Uhamisho wa wanafunzi na wafanyakazi unashughulikiwa hapa
hapa Wilayani Nyasa. Vibali navyo vipo vya kila aina.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Nyasa, mwanzoni alikuwa wa Halmashauri ya Mbinga.
Ni wakati bora kabisa huu kwani wilaya ilitakiwa kitambo sana
ReplyDelete