June 27, 2014

NANI RAIA HALALI?Na James Zotto, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM

Labda mimi pia niwape habari kama hii ya Mh. Msando Alberto: Kule kwetu Nyasa, kijiji na kata ya Liuli, kulitokea mzee mmoja anaitwa John John Mpembo Nyirenda. Hili jina linafana na koo za Malawi, Zambia, Msumbiji na Tanzania.

In short, koo nyingi za mwambao wa ziwa zinamchanganyiko wa nchi hizi na hata Swaziland, Lesotho na Afrika Kusini pia.Ni sawasawa tu na sehemu zingine zote za mipakani si Tanzania tu. 

Nimeandika chapter two ya thesis yangu kuhusu Social formation na peopling ya watu wa ziwa nyasa. Pia someni Seligman, Ehret, etc mtaona watu wa bara hii wamezungukaje/asili yao. 

Huyu Mzaee niliyemtaja alikuwa Mwanajeshi wa Jeshi Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Watu wa Tanganyika/Tanzania Bara. Alipostaafu, akarudi kijijini kwetu Liuli.

Kulikuwa na imani mzee mmoja alikuwa anafuga mamba. Ni kweli ziwa letu lilikuwa na mamba wengi, ila sijui ni wa Mungu au binadamu.Watu walikuwa wanauliwa sana na mamba. 

Huyu mwanajeshi mstaafu alisaidia kutega mitego, mamba wengi waliuawa. Tukawa tunaogelea kwa raha zetu. Huyu mzee alikuwa hataki kusikia uchawi, tena hasa kijana kalogwa, maana aliamini ndo nguzo ya Taifa na Liuli ya Nyasa. Kwa ukali wake, akabatizwa jina la MREMA.

Akifananishwa na Lyatonga Mrema wa Vunjo wa kipindi kile. Akagombea udiwani huyu mzee. Kampeni za nini? Alishinda kwa kura zote. Aligombea na binamu yake ambaye hawaelewani....wote asili yao Malawi.

Ukoo wa Kondowe! Huyu binanamu, inaaminika, akamchongea Uhamiajji kuwa Mh. Diwani wetu wa Nyasa si MTANZANIA. Nafikiri anamihela binamu huyu na nafikiri walidhani angegombea hata Ubunge.

Na angeshinda kweli. Eh...Uhamiaji wakafanya mambo. Wakamvua Uraia. Tukampoteza Diwani wetu kipenzi. Akaomba Uraia. Akapewa 'fasta'!
Msando, naomba usome hii habari, itakufariji na kuelewa nchi hii.

Sasahivi baba huyu kafa. Ulikuwa msiba wa aina yake. Si watu ni kama wingu hakuna pa kukanyaga, shujaa. Jiulize! Tulikuwa na mwanajeshi, tena mwenye kacheo, lakini si Mzawa....Hamuoni ni hatari?

Tulikuwa na Councillor lakini si mzawa, hamuoni hatari? ila kwa yote, yupi bora, huyu ambaye kaitwa si raia aliyepigania haki ya vijana, kaleta amani ama hawa wajiitao wazawa wachawi na waonevu na hawana la maana?

Lakini wote koo zao ni asili ya Malawi haimaanishi zimeanzia malawi. Alizaliwa Liuli, baba yake pia, mababu zao ndo walihamia.......La sivyo, chukua robo tatu ya Nyasa na uiondoe siujui uipeleke wapi sasa na ndivyo hata maeneo mengi ya mpakani na hata kati.

NANI RAIA WA NCHI HII? Naombeni jibu. Kama ndo hivyo, lile darasa letu la HGL-1998-2000 lililoongoza nchi nzima kwa matokeo na ambalo limetoa watu wataalamu wanaosaidia nchi hii, basi karibu lote linatokea mpakani, na hivyo si RAIA? I wanted to share this with you.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako