February 23, 2014

'BAY LIVE SOCIAL HALL' NA MASWALI KIBAO KWA WANYASA
Na Vitus Matembo, Mbamba Bay
 
Huu ni mwanzo tu wa hatua kufikia kilele. Ndugu yetu Madenge Chindogo kaanza hivi. Je wengine tunasubiri nini, mnawekeza tu mijini eeh!. Pengezo nyingi sana ndugu yetu huyu.
MAPROFESA 27; Wilaya ya Nyasa lakini Elimu Nyasa ni ya Mwisho. Kilosa na Chiulu ndio kumejaa maprofesa ila elimu yake majanga tu.

JAJI mstaafu B. Samatha tutakulilia sana ila Wanyasa hawatakusahau.
MJOMBA wangu wa damu, Luteni Jenerali C.L.MAKAKALA unacheo kikubwa sana. Tubebe ndugu zako wakinyasa hata Jeshini tu. Ndengele wanakulilia ulete maendeleo.

IGNATIO L. MATIMBA KOMBA, toka Tumbi. Nakuomba uje uwekeze Nyasa kielimu. Naheshimu sana nafasi yako ya ukaguzi kanda ya Kaskazini.
Kaka HOOPS KAMANGA, Rudi nyumbani uinue KILIMO Nyasa.
Mama STELLA MANYANYA kumbe ni mnyasa, usikusahau Nyasa.
HEBU TAJA WENGINE WENGI NA UELEZE NINI WAKIFANYE NYASA!!

1 comment:

  1. Hakika hii imenisononesha kusema ule ukweli. Hata hivyo sishangai kwani hii ni kama tabia sugu ya ndugu zangu wa kinyasa. Hata hivyo unaposema wanyasa unapaswa kuelewa kuwa kuna aina mbili yaani hao wa wilaya ya Nyasa na wale ambao ni wanyasa lakini walizaliwa na kukulia mikoa mingine kutokna na kukimbia utawala wa kiimla huko Malawi.

    ReplyDelete

Maoni yako