Na Egbart Jeremy,Mbamba Bay
Hatimaye shehena ya kwanza ya
Nguzo za Umeme iliwasilishwa Juni 20 mjini Mbambabay ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa kusambaza umeme vijijini pamoja na wilaya Nyasa ambayo ni mpya.
Kwa mujibu wa msimamizi wa mradi
huo, Bwana Hugo alisema kuwa licha ya ubovu wa barabara lakini walifanikwia
kuwasilisha shehena hiyo.
Alisema kuwa gari lilikuwa
linakwama mara kwa mara ana kutokana na vifusi vilivyowekwa ikiwa ni jitihada kubwa
zilizofanywa na Mbunge, John Komba kuwasiliana na maofisa wa TANROD mkoa wa Ruvuma
wamwamuru mkandarasi kusambaza vifusi.
Kwa mujibu wa msimamizi wa
mradi huo, alisema juhudi za kupeleka umeme wilaya ya Nyasa zimetokana na na mbunge huyo. Mradi huo ulitakiwa kuanzia
wilaya ya Tunduru lakini Mbunge Komba amejenga hoja hadi mpango ukabadilishwa
kuanzia wilaya ya Nyasa
No comments:
Post a Comment
Maoni yako