June 27, 2014

OFISI ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYASA ZIMEHAMIA KILOSA JENGO LA KILIMO
Na Vitus Matembo, Mbamba Bay
 
Ofisi za Halmashauri ya Nyasa zilizokuwa zimewekwa katika Lodge ya Mzee mmoja hapa Tambachi mjini Mbamba bay zimehama kwa lazima na kwenda katika Jengo la Kilimo katika mji wa Kilosa karibu na Limbo Sekondari.  

Hata hivyo, ofisi ya mkuu wa wilaya bado ipo hapa Mbamba bay lakini iko mbioni kuhamia huko Kilosa.  Sababu kuu za kuondolewa ofisi ya Halmashauri ni kudaiwa kodi kubwa na pia Kero kubwa toka kwa mmiliki. 

Mmiliki wa Lodge hiyo hakusamehe hata siku moja kwa malipo ya Lodge yake. Wafanyakazi hawakuruhusiwa kuokota hata maembe wala kuchuma katika eneo hilo walilopanga awali.

JE, wajua pia mzee huyo huwa anazamisha mitandao simu hapa Nyasa upande wa Kusini kama kampuni zimechelewa kumlipa fidia au Kodi. Na twaweza kukaa hata wiki bila mawasiliano na kulazimika kwenda ziwani kupata mtandao toka Liuli?

1 comment:

Maoni yako