September 30, 2014

NAFASI ZA KAZI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI BAADA YA SIKU 14.
*JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*
*WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI*
*TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI*
*2. KONSTEBO WA UHAMIAJI Nafasi 114 - (Nafasi 100 kwa ajili ya* *Tanzania Bara na Zanzibar na nafasi 14 maalum kwa ajili ya Zanzibar tu)*
A. SIFA ZA MWOMBAJI:
(i) Awe Raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 20 hadi 25.
(ii) Awe amehitimu kidato cha nne na kufaulu masomo ya Kiingereza,
Kiswahili, Historia, Jiografia, Kifaransa, Hisabati ambapo masomo matatu
kati ya hayo yawe katika kiwango cha Credit
(iii) Awe pia na mojawapo ya sifa zifuatazo:
Cheti cha Sheria;
Cheti cha Utunzaji Kumbukumbu;
Cheti cha Kompyuta;
Cheti cha Ufundi (FTC);
Cheti cha Mafunzo ya Ufundi Stadi kwenye fani ya (umeme, mitambo, bomba);
(iv) Waombaji wenye ujuzi wa mojawapo ya lugha zifuatazo (Kifaransa,
Kichina, Kijerumani, Kiarabu au Kihispania) watafikiriwa kwanza.
(v) Aidha, Mwombaji aliyepitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa atapewa
kipaumbele.
B. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
(i) Kupanga majalada ya watumiaji wa huduma za uhamiaji;
(ii) Kufungua na kutunza majalada yenye orodha ya majina ya watumiaji wa
huduma za uhamiaji;
(iii) Kufanya doria sehemu za mipakani, bandarini, vituo vya mabasi,
treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini;
(iv) Kukamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya uhamiaji na kuwafikisha
kwenye mamlaka husika;
(v) Kufanya ukaguzi kwenye hoteli, nyumba za kulala wageni na sehemu za
biashara;
(vi) Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za uhamiaji mahakamani pamoja na
wageni wanaofukuzwa nchini (Deportees)
(vii) Kufanya matengenezo/ukarabati wa mitambo na vitendea kazi vya
uhamiaji;
(viii) Kuandaa hati mbalimbali za uhamiaji.
3. UWASILISHAJI WA MAOMBI
Barua za maombi zinapaswa kuandikwa kwa mkono na kuwasilishwa kwa njia
ya posta zikiwa zimeambatishwa na:-
(i) Nakala ya cheti cha kuzaliwa;
(ii) Nakala ya cheti cha kuhitimu masomo ya sekondari pamoja na vyeti
kwa mujibu wa sifa nyingine zilizoainishwa kwenye kipengele A(iii).
(result slips hazitakubalika)
(iii) Nakala ya vyeti vya kumaliza shule ya msingi na sekondari (Leaving
Certificates);
(iv) Picha mbili (Passport Size);
(v) Barua ya Utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za
Mitaa/Shehia/ Vijiji;
(vi) Nakala za vyeti vyote vitakavyowasilishwa viwe vimethibitishwa na
Wakili/ Kamishna wa Viapo.
4. ANUANI YA KUWASILISHA MAOMBI
Barua za maombi ya kazi ziwasilishwe kwa njia ya posta ndani ya kipindi
cha siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili kwa anuani zifuatazo:-
Waombaji wa nafasi 200 (100 Koplo na 100 Konstebo) ambazo ni kwa ajili
ya Tanzania Bara na Zanzibar wawasilishe maombi yao
kwa anuani ifuatayo:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
S.L.P 9223,
DAR ES SALAAM.
Waombaji wa nafasi 28 (14 Koplo na 14 Konstebo) ambazo ni maalum kwa
Zanzibar wawasilishe maombi yao kwa anuani ifuatayo: Katibu Mkuu,Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
C/O Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,
S.L.P 1354,
ZANZIBAR.
Maombi ambayo hayatazingatia maelekezo tajwa hapo juu hayatashughulikiwa.
CHANZO: DAILY NEWS LA TAREHE 29 SEPTEMBA 2014

No comments:

Post a Comment

Maoni yako