September 29, 2014

USAJILI WA CHAMA CHA WALIOHITIMU SEKONDARI YA LUNDOJumamosi tarehe 27.09.2014 Msimbazi Centre-Dar es Salama kilifanyika kikao cha wanajamii wote waliosoma katika sekondari ya Lundo.

TAARIFA zinasema kuwa,  kikao kilikwenda vyema sana. Wajumbe waliokuwepo wamekubaliana kukamilisha mchakato wa kusajili chama wahitimu wa Lundo Sekondari " LUNDO SECONDARY SCHOOL ALUMNI" . 

Kikao kingine kitafanyika siku ya jumamosi tarehe 4.10.2014  ikiwa na lengo la kukamilisha kusaini nyaraka husika za usajili.
Aidha, ili kuwezesha wenzetu waliopo mikoani kushiriki kwenye suala hili, Katiba yetu itatambua "Chapters" kwa mikoa tofauti ambapo wale walio nje ya Dar es salaam wataweza nao kukutana kama ilivyo kwa Dar. 

Mpaka kikao cha leo tumeweza kukusanya jumla ya kiasi cha Tshs. Laki Nne (400, 000 ) kutoka kwa wajumbe walioguswa, tunawashukuru sana.
Tunaendelea kuwahamasisha wote.... tuendelee kushirikiana. 

Kwa wale watakaoguswa tulikubaliana kikao cha kwanza kuwa tuendele kuwasilisha michango yetu kwa Mhazini (0715008688). Kwa lengo la awali, tunaangalia upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na tutaendelea kwenye hatua ya pili ya kushughulikia ukarabati wa majengo kwa kadri tutakachopata.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako