September 20, 2017

ELIMU LAZIMA IWE HALISI NA INAYOGUSA HISIA

NA SAMWEL CHITANYA, SONGEA
WEWE ni mtanzania umefundishwa mambo mengi kutoka kwa wazazi,walezi na walimu wako. Jitahidi kuyakumbuka unayofundishwa na uyalete katika maisha ya kila Siku.  Wale waliokufundisha mambo mbalimbali walikupa msingi wa jengo tu. Sasa ni jukumu lako kumaliza nyumba, paa na sakafu. Tumia akili yako kuyaendeleza uliyofundishwa na jamii yako na darasani. 

Elimu ya kukariri imepitwa na wakati, umombo au ung'eng'e kama mnavoita, unakwamisha urithishwaji au uhamishwaji wa elimu kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Nchi inaendelea kuwa na wasomi wengi lakini wenye uelewa mdogo wa mambo mbalimbali ukilinganisha na viwango vya elimu vilivyo andikwa kwenye vyeti vyao (Tuna wasomi wengi wa kwenye makaratasi kuliko maarifa na ujuzi halisia wa jambo husika walilosomea). Ndio maana haishangazi kuona unaumwa mguu una pasuliwa kichwa.

Elimu yetu lazima iwe halisi na yenye kugusa hisia, tukifanya hivo tutafika kule tunakotaka kufika, lakini kwa elimu hii ya kukariri na umombo sioni kama ni kwa namna gani tutafika huko. Tunajichelewesha wenyewe kwa kuendekeza na kuaminishana kuwa ili uwe msomi mzuri lazima ujue kimombo.

Ni wakati wa kuamua Kiswahili kitumike katika ngazi zote za elimu kama lugha ya kufundishia kama kweli tunahitaji wataalamu wanao endana na elimu zilizo andikwa kwenye vyeti. #1820.

©Nishani MEDIA
Songea,
Juni 21, 2017

No comments:

Post a Comment

Maoni yako