HISTORIA ya kivutio cha utalii,
kisiwa cha Lundo kilichopo Ziwa Nyasa, inaonesha kuwa kisiwa hicho kina ukubwa
za hekta 20 kimepewa jina la Lundo kwa sababu watu wa kwanza waliovuka kisiwa
hicho kwenda ng’ambo ya pili walifikia kijiji cha Lundo.
Kisiwa hicho tangu zamani
kilikuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa vijiji vya Lundo,Ngindo na Chinula
kwa sababu wakati wa vita ya Majimaji vilivyotokea kati ya mwaka 1905 hadi 1907
watu walikuwa wanakimbilia katika kisiwa hicho ambacho kina maeneo ya maficho.
Baada ya vita ya Majimaji
kuanzia mwaka 1908 kisiwa hiki kilitumika na wakoloni wa kijerumani kuwahifadhi
watu waliopata ulemavu kutokana na ugonjwa wa ukoma ambao baada ya uhuru
walihamishiwa katika makazi ya Ngehe wilayani Nyasa. Serikali imependekeza
visiwa vya Lundo na Mbamba Bay kuwa hifadhi za wanyamapori.
Visiwa hivyo vitakuwa ni
hifadhi ya pekee ya wanyamapori pamoja na samaki wa mapambo wanaozaliana katika
visiwa hivyo ndani ya ziwa Nyasa hivyo kuvutia watalii kufika kusini na
kutekeleza Sera ya nchi ya kufungua biashara ya utalii Kusini.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako