Na Honorius Mpangala
ORGENESS
Mollel ni moja ya vijana wa kitanzania wanaocheza soka Ulaya. Ni katika klabu
ya Famalecao ya Ureno ndiko anakocheza kijana huyu Wa kitanzania. Kwa kipindi
amacho kocha Mkuu Wa taifa Stars Salum Mayanga amekuwa muumini Wa kuwapa nafasi
wachezaji wanaocheza soka nje ya Tanzania. Jambo afanyalo Kocha huyu unaweza
kusema kama ni chachu ya kuthamini uwezo Wa wachezaji hao wanaowakilisha taifa
letu nje ya mipaka ya Tanzania.
Kwa
Mara ya kwanza kocha wa Taifa stars anamjumuisha Mollel nilijikuta natamani
kufahamu mengi toka kwake. Hamu hiyo ilikuja baada ya kufahamika hatoweza
kujiunga na timu kutokana na kibali chake anachotumia kuto mruhusu kutoka na
kuingia kwa kutumia kibali hicho. Niliifuatilia hati ya kuzaliwa ya Mollel na
kugundua anatumia hati ya Tanzania na kumwonyesha ana umri Wa miaka kumi na
tisa. Nilikuja kushangazwa zaidi alipoitwa kwa Mara nyingine na kushindwa
kuungana na wenzake kwa Mara ya pili.
Waweza
kusema kila mmoja na anabahati yake kama ilivyo kwa Mollel. Bahati ya Mollel
yawzekana wako watu kama Emily Mgeta kule Ujerumani wanaitazama kwa jicho la
matamanio sana. Sio kama kila mmoja ataweza kuushawishi uongozi Wa benchi la
ufundi liweze kukujumuisha katika timu ya taifa. Kinachofanyika ni kufuatiliwa
kwa mchezaji ndiko kunakoweza kutoa majibu kuwa maendeleo yake yakoje ili aweze
kuitwa.
Iliwahi
kutokea kwa Adam Nditi ambaye mwaka 2013 alikuwa katika timu ya vijana ya
Chelsea akikumbana vikumbo na Paul Pogba,Nathan Ake,Gael kakuta,Adnan Januzaj
na vijana wengine Wa vilabu vya ligi kuu nchini Uingereza. Wakati matamanio ya
wapenzi wengi walitamani kumwona katika jezi ya timu ya taifa Nditi aliyeyuka
kama barafu katika maji ya uvuguvugu. Hadi leo hakuna kocha anayetamani hata
kufahamu Nditi yuko wapi kwa sasa. Miongoni mwa mambo yaliyopelekea kuachana na
kijana huyo ilikuwa baada ya kubainika hati ya kusafiria anayotumia
inamtambulisha kama Mwingereza na sio Manzania tena kama ilivyotarajiwa na
wengi.
Nafasi
aliyoitoa Mayanga kwa Mollel inaweza kuwatazama wengine. kwasababu hadi sasa ni
kama Klabu yake ya famalecao haitoi ushirikiano na Tanzania pale wanapomhitaji
kijana huyo anapoitwa timu ya taifa.
Nchini
Austria kuna kijana Wa kitanzania ambaye ana matamanio sana ya kuja kuitumikia
nchi yake. Ni Thomas Lema ambaye ana umri Wa miaka 17 tu. Amekuwa na wakati
mzuri sana katika klabu Yale kwani licha ya kuwa na hati ya kusafiria ya
Austria lakini kwa umri wake hazuiliwi kuchagua timu anayotaka
kuichezea.Iliwahi kutokea kwa Fredrick Kanoute,Karim Zian na wengine ambao
waliwahi kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa lakini baadaye wakaamua kuchagua
kuichezea timu ambayo ni ya Asili yao.Haikushangaza kumwona Kanoute akikipiga
katika nchi ya Mali na Karim Ziani akikipiga Algeria.
Ni
wakati Wa kuwafuatilia vijana wote wenye hati za kusafiria za kitanzania.
Katika nchi ya Afrika kusini kuna vijana kama Jaffary Kapolo Wa Real Kings
daraja la kwanza. Ni moja ya vijana ambao naamini kama watapewa nafasi ya
kujumuishwa tu katika kikosi itakuwa ni 'credit' kwa timu yake na yeye mwenyewe
nankuaminika katika klabu.
Ujerumani
licha ya kuwepo kwa Emily Mgeta ambaye hucheza nafasi ya ulinzi daraja la tano
katika klabu Freund Spiel Lauffen pia kuna Mtanzania mwingine aitwaye Charles
Mishetto aliyeko katika klabu ya daraja la nne inayoitwa S.P.B.G 1914 Selbitz.
Yawezekana kama tumeegemea katika kuwafahamu Simon msuva na wenzake ambao
kiuchezaji wameanzia nyumbani Tanzania. Lakini tujaribu kuwafuatilia vijana
wetu yawezekama huko waliko vilabu yao vikatamani kuona wakiitwa timu zao za
taifa.
Hamis
Mroki ni mmoja ya vijana ambao Kocha Jamhuri kihwelo aliwahi kuwajumuisha
katika kikosi cha taifa kwa vijana Wa umri Wa chini ya miaka 23. Mroki ni
mchezaji Wa ligi daraja la pili nchini Thailand akiichezea klabu ya Kabin
United. Huyu tayari alikuwa na mwanzo mzuri ambao kwani tayari alishavaa jezi
ya taifa katika u23 kwenye mechi dhidi ya Kameruni.
Yawezekana
kila mmoja huandikiwa njia za kufanikiwa lakini ufuatiaji kwa vijana wa
kitanzania ni jambo muhimu kwetu. Haiwezi kuwa na faida yoyote kama tutaishia
kujisifu kwa kumwona Saidi Mhando akija kucheza ligi kuu Italia toka daraja
alilokuwa sasa seria B na klabu yake ya Brescia Calcio.
Maana
yawezekana hata wao huweza kufikia maamuzi kama yakiyokwisha fanyika kwa baadhi
ya wachezaji kuzikacha nchi zao na kuchezea mataifa mengine ambayo yamewainua
kimpira. Ilitokea hivyo kwa Edson De
Souza 'Deco' na mlinzi matata Pepe ambao waliichezea Ureno badala ya Brazil.
Labda
nikujuze jambo moja kuna kijana mmoja wa kitanzania ambaye hufahamika kwaji
moja LA Faheem alifanikiwa kusainishwa na klabu ya Sporting Lisbon ya vijana
akiwa na miaka 19. Ni kijana wa kitanzana lakini inasemekana tayari wareno
wamempa uraia huku wazazi wa kiana huyo wakiwa Watanzania. Tuna kila sababu ya
kuwalinda vijana wetu Kwa kuwajumuisha katika kikosi cha timu ya taifa.Ni vyema
mwalimu Wa timu ya taifa akajaribu kufuatilia hata TFF kutazama ni wachezaji
gani ambo wako nje na wamepewa vibali vya kucheza huko na shirikisho ili kuweza
kuleta urahisi Wa kuwafuatilia.
Kila
mpenzi Wa soka nchini Tanzania atakuwa na kumbukumbu ya mchezo Wa Yanga dhidi
ya Zanaco. Kijana Wa kitanzania Ayoub Lyanga ambaye ni mdogo Wa Danny Lyanga
aliingia akitokea benchi na kushirikia katika mchezo huo Wa ligi ya mabingwa.
Lyanga ni kijana aliyecheza katika klabu ya African sports kabla hajaenda
kufanya majaribio katika klabu hiyo na kufanikiwa kusajiliwa na Zanaco. Moja ya
mambo yaliyo nishangaza ni pale nilipotembelea tivuti ya klabu ya Zanaco na
kuona katika orodha ya Wachezaji wao Lyanga kawekewa Bendera ya Zambia
ikimtambulisha kama ni raia wa Zambia.Suala la kufuatilia maendeleo ya mchezaji
lazima liwe kwa mgawanyo Wa majukumu ili kuleta ufanisi wa uteuzi Wa timu
taifa.
Tujaribu
kutoa nafasi kwa watu wengine zaidi na zaidi ili kuonyesha tunahazina kubwa ya
wachezaji walioko nje. Itafurahisha na kuwafanya wapenzi Wa soka wajivunie
uwepo Wa vijana kama George Mtemahanji anayekipiga daraja la pili katika klabu
ya Modena fc pale Italia,Golikipa Abasi Pira,Hassan Sembi ambao kwa namna moja
au nyingine wanaweza kutoa changamoto kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani.
Wakiwa
wananolewa na Milutin Sredojovic Micho,timu ya taifa ya Uganda waliamua
kumwachia fungu la pesa kama nauli ili kuweza kusaka wachezaji wenye asili ya
uganda na kuwatambua na hatimaye kujumuishwa timu ya taifa. Michu alifika hadi
katika nchi kama Lebanon akawakuta wachezaji Wa Uganda na hata katika taifa la
Vietnam na wachezaji wake walikuja kuwa msaada Wa timu ya Uganda hadi akafuzu
kucheza Afcon pale Gabon.
Hata
Siku moja daraja la nne katika nchi ya Ujerumani haiwezi kufanana kiuendeshaji
Wa klabu Sawa na ile klabu ya ligi kuu Tanzania. Miundombinu hadi utawala
lazima vitakuwa tofauti kwasababu wenzetu wanatambua umuhimu Wa madaraja hayo
kwani ni chachu ya kuwapata wachezaji wazuri.
Kama
famalecao hawakutoa ushirikiano kwa Tanzania ili kumtumia Orgeness Mollel
katika timu ya taifa. Ni nafasi sasa kwa vijana wengine kutoka nje kuna
kuitumikia nchi yao. Nimefurahishwa na Kujumuishwa kwa Yohana Nkomola pamoja na
Dickson Job vijana hawa Wa timu ya vijana wamenifanya nikumbuke nyakati ambazo
Kocha Mbrazil Marcio Maximo alipokuwa akiwajumuisha Jerry Tegete na Kiggy
Makasi. Akaja pia kuwa na utaratibu Wa kuwajumuisha Himid Mao ,Omega Seme na
Thomas Ulimwengu. Kuwajumuisha vijana hao huleta faida baada kwa taifa kwani
tumeona kwa Tegete,ulimwengu na Himid walivyokuja kulisaidia Taifa hili kwa
vipindi tofauti.
Watanzania
waonapo vijana kama Abdul Mohammed toka Tusker na Hamis Abdallaha wakijiunga
taifa stars kwa kuwasili uwanja Wa ndege wa Mwalimu Julius K Nuerere inatia
hamasa. Hata wachezaji wenyewe wanaona sasa ile thamani yetu ya kucheza nje ya
mipaka ya nchi yetu inaonekana. Kila
la kheri Mayanga katika maandalizi yako dhidi ya Benin. Watanzani wote wako pamoja
nanyi katika kuwaombea na kuwatakiwa mambo mazuri.
0628994409
No comments:
Post a Comment
Maoni yako