NA MARKUS MPANGALA
JIWE hili ni maarufu sana katika kijiji cha Lundu. Linaitwa Kinanda au kwa wenyeji tunaliita kienyeji “Chinanda”. Lipo katika forodha ya Chivanga. Picha hii ilipigwa mapema Mwezi Februari mwaka huu.
JIWE hili ni maarufu sana katika kijiji cha Lundu. Linaitwa Kinanda au kwa wenyeji tunaliita kienyeji “Chinanda”. Lipo katika forodha ya Chivanga. Picha hii ilipigwa mapema Mwezi Februari mwaka huu.
Honorius Mpangala akiwa katika Jiwe la Kinanda, Februari mwaka huu. |
Lipo
jambo moja la kusikitisha ni kwamba kiasi cha Maji katika Ziwa Nyasa si kama
kile kilichokuwa zamani. Katika miaka ya 1980 hadi miaka 90 jiwe hilo
lilizungukwa na Maji. Lakini miaka mwanzoni mwa 200o kumekuwa na mabadiliko
mengi katikam ziwa.
Katika
miaka 1980 na 90 hiakuwa kazi rahisi kulifikia jiwe hilo. Lilizungukwa na maji
kila upande, palikuwa na kina kirefu kiasi chake. Lakini sasa hali ni tofauti
sana, kwani lipo mbali na maji kama linavyoonekana pichani. Ni ishara ya wazi
kuwa maji ya Ziwa Nyasa yanapungua siku hadi siku.
Wataalamu wa masuala hayo wanaweza kutueleza kuwa huenda ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Yapo maeneo
mengine ambayo maji yamehama kabisa, wakati miaka ya nyuma yalizungukwa na
maji. Ni jambo ambalo linahitajika kufanyika utafiti zaidi wa kitaalamu kubaini
nini kinachosababisha hali ya kupungua maji.
Ikumbukwe
Maji ya Ziwani ni tofauti na bahari ambako yanahama na kurudi. Lakini ziwani
maji huondoka moja kwa moja. Hata kipindi cha masika mvua haziongezi maji mengi
licha ya maji kuongezeka wakati fulani.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako